Pata taarifa kuu
MOROCCO-AMNESTY-HAKI

Morocco yapinga ripoti ya Amnesty International kuhusu mwandishi wa habari Omar Radi

Mamlaka nchini Morocco imefutilia mbali madai ya shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International kwamba ilimpeleleza Omar Radi, mwandishi wa habari anayejulikana nchini humo kwa kujitolea katika kutetea haki za binadamu, kwa kutumia kifaa kilichoandaliwa na kampuni ya Israeli ya NSO Group.

Kulingana na ofisi ya mashitaka, Omar Radi (kwenye picha) alihojiwa na polisi Alhamisi wiki hii kwa madai ya kupokea pesa kutokana na kazi aliyoifanya kwa niaba ya idara za ujasusi za kigeni.
Kulingana na ofisi ya mashitaka, Omar Radi (kwenye picha) alihojiwa na polisi Alhamisi wiki hii kwa madai ya kupokea pesa kutokana na kazi aliyoifanya kwa niaba ya idara za ujasusi za kigeni. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Amnesty International, simu ya rununu ya Omar Radi ilishambuliwa mara kadhaa, mashambulizi ambayo yaliwezesha kuingizwa kwenye simu hiyo programu ya kijasusi iitwayo Pegasus, iliyotengenezwa na kampuni ya Israeli ya NSO Group.

Katika taarifa iliyorushwa na vyombo vya habari nchini Morocco, mamlaka nchini humo imesema kwamba Amnesty haijawasiliana nao na kwamba ripoti ya shirika hilo inaangazia masilahi ya washindani wa kampuni ya NSO Group kwenye soko la teknolojia ya ujasusi.

Mamlaka nchini Morocco imeliomba shirika la Amnesty International kutoa ushahidi kamili kuhusu madai yake ili iweze kuchukua hatua muhimu kwa kutetea haki za wananchi wa Morocco.

Kulingana na ofisi ya mashitaka, Omar Radi alihojiwa na polisi Alhamisi wiki hii kwa madai ya kupokea pesa kutokana na kazi aliyoifanya kwa niaba ya idara za ujasusi za kigeni.

Mwandishi huyo wa habari alikataa kujieleza kuhusu madai hayo, lakini alisema kuwa madai hayo hayana msingi wowote.

Mnamo mwezi Machi Omar Radi alihukumiwa kifungo cha miezi minne jela kwa kumdharau hakimu kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.