Pata taarifa kuu
MOROCCO-SIASA-USALAMA

Morocco: Waziri Mkuu wa zamani Abderrahmane Youssoufi afariki dunia

Abderrahmane Youssoufi, ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa Morocco kati ya mwaka 1998 na 2002, amefariki diunia jana usiku huko Casablanca, ambapo alikuwa amelazwa hospitalini tangu Jumapili. Alikuwa na umri wa miaka 96.

Waziri Mkuu wa zamani wa Morocco Abderrahmane Youssoufi, Machi 2018.
Waziri Mkuu wa zamani wa Morocco Abderrahmane Youssoufi, Machi 2018. STR / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kifo chake kimethibitishwa na shirika la Habari la Morocco na Waziri Mkuu Saad Eddine el-Othmani kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Huko Tangier, mji ambapo Abderrahmane Youssoufi alizaliwa mnamo mwaka 1924, kuna mtaa uliopewa jina lake. Mtaa huo ulizinduliwa na Mfalme Mohamed VI mnamo mwaka 2016. Abderrahmane Youssoufi pia alikuwa kiongozi wa serikali wakati Mfalme wa sasa wa Morocco alichukua hatamu ya uongozi wa nchi mnamo mwaka 1999.

Mwaka mmoja kabla, mnamo mwaka 1998, baba yake Mohamed VI, Mfalme Hassan II, alimteua kuunda "serikali ya maridhiano", baada ya kuwashirikisha wanasiasa wa mrengo wa kushotokutoka kambi ya upinzani. Wakati huo Hassan II alijiua kuwa anataka kuachia ngazi na kuandaa mabadiliko na mwanae kumrithi. Kazi hiyo kubwa ilikabidhiwa Abderrahmane Youssoufi, mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa kutoka mrengo wa kushoto, na mmoja wa vigogo wa chama cha USFP, ambaye alikuwa katibu wa kwanza kwa miaka kumi, hadi mwanzoni mwa mwaka wa 2000.

Mwandishi mmoja wa habari wa zamani wa Morocco anamueleza kama mtu mkweli na mwaminifu, ambaye hajawahi kwenda kinyume na maadili yake.

Aderrahmane Youssoufi aliwahi kuwa Waziri Mkuu hadi mwakla 2002. Kuondoka kwake serikalini, ikifuatiwa miezi michache baadaye na kujiuzulu kwake nafasi ya katibu wa kwanza wa chama cha USFP, kulikuja baada ya kustaafu katika ukumbi wa siasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.