Pata taarifa kuu
MOROCCO-CORONA-AFYA

Coronavirus: Morocco yaagiza raia wake kuvaa barakoa

Morocco imetoa agizo kwa raia wake kuvaa mask kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vibavyo sababisha ugonjwa hatari wa Covid-19, ambao Umoja wa Mataifa uliutaja kuwa ni janga la kimataifa.

Serikali ya Morocco imeagiza raia wake kuvaa mask kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.
Serikali ya Morocco imeagiza raia wake kuvaa mask kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Morocco imebaini kwamba kuvaa barakoa ni lazima kwa mtu yeyote anayeruhusiwa kuondoka nyumbani kwao wakati janga la Covid-19 likiendelea kusambaa kwa kati katika maeneomnali duniani.

"Mtu yeyote anayeruhusiwa kuondoka nyumbani kwao ni lazima avae barakoa kwa kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona wakati huu; " serikali imesema.

Serikali ya Morocco imeonya kwa wale ambao watakadi agizo hilo kwamba watakabiliwa ni kifungo cha miezi mitatu.

Watu 1,120 wameambukizwa virusi vya Corona, huku ugonjwa huo ukisababisha vifo vya watu 80. raia wa nchi hiyo wameendelea kubaki nyumbani.

Uwezo wa uzalishaji wa mask kwa siku utaongezwa hadi karibu milioni 6 wiki ijayo, ikilinganishwa na milioni 3.3 hivi sasa, msemaji wa Wizara ya Viwanda ameliambia shirika la habari la Reuters.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.