Pata taarifa kuu
UFARANSA-USHIRIKIANO

Emmanuel Macron afuta ziara yake ya kwenda Mali kwa sababu ya Covid-19

Ikulu ya Élysée ilitangaza Ijumaa hii, Desemba 17, 2021 kwamba rais wa Ufaransa hatoweza kwenda nchini Mali kukutana na rais wa mpito na kusherehekea Krismasi na wanajeshi wa Ufaransa. Kufutwa kwa ziara hiyo kunatokana na ugonjwa wa Covid-19 unaosambaa kwa kasi kubwa nchini Ufaransa.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akiwa na Waziri wa Afya Olivier Véran, Machi 2021 huko Créteil.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akiwa na Waziri wa Afya Olivier Véran, Machi 2021 huko Créteil. AP - Ludovic Marin
Matangazo ya kibiashara

Paris ilitangaza wiki hii kwamba Emmanuel Macron atakwenda Bamako siku ya Jumatatu kukutana kwa mara ya kwanza na Kanali Assimi Goïta, rais wa mpito wa Mali, katika hali ya mvutano mkali kati ya Ufaransa na utawala wa kijeshi.

Uamuzi wa kufuta ziara hii "ulichukuliwa kwa ajili ya uthabiti kati ya hatua zilizotangazwa katika ngazi ya kitaifa na ajenda ya kimataifa ya rais, na kwa ajili ya kutoweka wazi mfumo wetu wa kijeshi wakati wa kuzorota kwa hali ya afya nchini Ufaransa, " Elysée imebaini.

Tangazo hilo lilitolewa baada ya kufanyika kwa Baraza la Ulinzi la Afya, lililokutana Ijumaa hii mjini Paris likiongozwa na rais Emmanuel Macron kuchunguza hatua mpya zinazotakiwa kutekelezwa dhifi ya mlipuko wa tano wa Covid, nchini Ufaransa. Waziri Mkuu Jean Castex alitangaza hatua hizi kwa wananchi baada ya mkutano.

Mjumbe kutoka Ufaransa alitangaza rasmi kwa mamlaka ya Mali kufutwa kwa ziara hiyo, kwa mujibu wa mshirika wa karibu wa rais wa mpito, Kanali Assimi Goïta. Chanzo hicho kinaongeza kuwa sababu iliyotolewa ni hatua zilizochukuliwa nchini Ufaransa siku hiyo kwa sababu ya janga la Covid-19, ameripoti mwandishi wetu huko Bamako, Serge Daniel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.