Pata taarifa kuu

Ufaransa yapiga marufuku safari zisizo za lazima kwenda na kutoka nchini Uingereza

Serikali ya Ufaransa, imetangaza kuzuia safari zisizo za lazima kwenda na kutoka nchini Uingereza kuanzia mwishoni mwa wiki hii, kufuatia kusambaa kwa kasi kwa kirusi kipya cha Covid-19, Omicron.

Uwanja wa ndege wa Paris, Roissy Charles De Gaulle.
Uwanja wa ndege wa Paris, Roissy Charles De Gaulle. Dmitry Avdeev/wikimedia.org
Matangazo ya kibiashara

Kuanzia saa sita usiku, siku ya Jumamosi hatua hiyo ya serikali ya Ufaransa itaanza kutekelezwa ikiwalenga watu wote, waliochanjwa na wasiochanjwa.

Aidha, serikali ya Ufaransa imesema, raia wa nchi yake, na wale kutoka mataifa ya Umoja wa Ulaya, wanaweza kurejea nyumbani wakitokea nchini Uingereza.

Pamoja na hilo, abiria wanaowasili nchini Ufaransa, watatakiwa kuwa na cheti cha kuonesha kuwa hawana maambukizi, baada ya kupima kwa muda wa saa 24, lakini pia watawekwa karatini.

Msemaji wa serikali ya Ufaransa Gabriel Attal amesema uamuzi huu wa serikali, unalenga kupunguza kasi ya kirusi hicho cha Omicron kufika nchini humo wakati huu serikali inapoendelea kuwahimiza wananchi kuchoma dozi ya tatu.

Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa msimamo huu wa serikali ya Ufaransa, umechangiwa kwa kisiasi kubwa kufuatia mvutano uliopo kati ya Paris na London kuhusu wahamiaji haramu na uvuvi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.