Pata taarifa kuu

Urusi yadai kuteka kijiji kipya mashariki mwa Ukraine

Jeshi la Urusi limedai siku ya Alhamisi kukiteka kijiji kipya mashariki mwa Ukraine, likiendelea kusonga mbele hatua kwa hatua katika eneo hili karibu na mji wa Avdiivka, uliotekwa na Moscow mnamo mwezi wa Februari. 

Mapigano yamekuwa yakipamba moto huko Avdiivka, kati ya bikosi vya Urusi na vile vya Ukraine.
Mapigano yamekuwa yakipamba moto huko Avdiivka, kati ya bikosi vya Urusi na vile vya Ukraine. AP - Libkos
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya Urusi " vimekomboa kabisa kijiji cha Berdychi," Wizara ya Ulinzi imesema katika taarifa yake ya kila siku. 

Siku ya Jumapili, Ukraine ilibaini kwamba ilikuwa ikiwaondoa wanajeshi wake magharibi mwa eneo hili.

Hayo yanajiri wakati watu watano wameuawa baada ya Urusi kufanya mashambulizi katika maeneo ya mashariki mwa Ukraine ya Kharkiv na Donetsk. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa mamlaka katika maeno hayo.

Gavana wa eneo la Kharkiv, Oleg Synegubov amesema katika eneo hilo lenye kupakana na Urusi, bomu liliwauwa watu wawili na wengine sita wakijeruhiwa akiwemo mtoto wa umri wa miaka 11.

Pamoja na ripoti za visa vya mauwaji mengine katika eneo la upande wa mashariki zaidi katika mkoa wa Kharkiv karibu na mji wa Kupiansk, makombora ya Urusi yamemuua mwanamke wa umri wa miaka 67 katika kijiji cha Lelyukivka.

Eneo hilo ambalo sehemu kubwa zinadhibitiwa na vikosi vya Urusi kwa miezi kadhaa baada ya uvamizi wake mnamo mwezi wa Februari 2022, linakabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.