Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi nchini Uingereza: Sadiq Khan achaguliwa tena kuwa meya wa London

Sadiq Khan amekuwa afisa wa kwanza kuchaguliwa kushinda umeya wa London kwa muhula wa tatu Jumamosi Mei 4. Lakini zaidi ya matokeo haya, chaguzi hizi za serikali ya mitaa zinaashiria ushindi mkubwa kwa chama cha Labour, miezi michache kabla ya uchaguzi wa wabunge.

Sadiq Khan atoa hotuba baada ya kuhesabiwa kwa kura huku akichaguliwa tena kuwa Meya wa London kwa mara ya tatu, London, Uingereza, Mei 4, 2024.
Sadiq Khan atoa hotuba baada ya kuhesabiwa kwa kura huku akichaguliwa tena kuwa Meya wa London kwa mara ya tatu, London, Uingereza, Mei 4, 2024. © AP - Alastair Grant
Matangazo ya kibiashara

Sadiq Khan, amemzidi mpinzani wake kutoka chama cha Conservative Susan Hall katika maeneo ya Labour ya mashariki na kusini mwa London. Alipata kura zaidi ya milioni moja kwa 43.8% ya kura zilizopigwa, zaidi ya pointi kumi na moja zaidi ya mshindani wake. Katika hotuba yake baada tu ya kutangazwa kwa matokeo, amesema "amevikwa taji" na "ana furaha" na akasema anatumai kuwa mwaka huu ungekuwa wa "mabadiliko makubwa" na "serikali ya baadaye ya Labour". Pia amesifu katika ushindi wake, ule wa kampeni ambayo ilitetea "mji ambao unaona utofauti wetu si udhaifu lakini kama nguvu inayoimarika, ambayo inakataa ubepari na kusonga mbele".

Sadiq Khan, 53, mtoto wa dereva wa basi, alishinda nafasi ya meya wa London kwa mara ya kwanza mwaka wa 2016. Kisha akawa Mwislamu wa kwanza kuongoza mji mkuu wa nchi hii ya Magharibi. Kwa muhula huu wa tatu, anashinda kwa suala la maisha marefu mtangulizi wake, Boris Johnson kutoka chama cha kihafidhina, aliyechaguliwa mara mbili.

Kwa muhula wake wa kwanza, Sadiq Khan alipigana kwa nguvu na kutaka Uingereza ijiondoka katika Umoja wa Ulaya, Brexit. Wakati huu, ameahidi jiji ambalo “litakuwa la haki zaidi, salama, na la kijani kibichi kwa kila mtu.” Anataka kupanua programu yake ya chakula cha mchana bila malipo kwa watoto wa shule za umma. Mwanamume huyo ambaye alikulia katika makazi ya kijamii, huko Tooting kusini mwa London, ameahidi kuwa nyumba mpya za kijamii 40,000 zitajengwa. Ameahidi kuchukua hatua ili kuhakikisha kuwa hakuna watu wasio na makazi tena London ifikapo mwaka 2030.

Mwanamume huyo, ambaye anachukuliwa kuwa hana mvuto, amekuwa msumbufu wa vyombo vya habari vya kihafidhina na Tories, madarakani nchini Uingereza tangu mwaka 2010. Wanamshambulia bila kuchoka kwa usalama. Wanamtuhumu kuhusika na ongezeko la mashambulizi ya visu, janga ambalo Sadiq Khan analihusisha kwa upande wake na sera ya kubana matumizi ya serikali za kihafidhina ambayo ingesababisha kupunguzwa kwa idadi ya polisi.

Wapinzani wa Sadiq Khan pia wanamtuhumu kwa kuongeza zaidi mwaka jana ushuru wa magari yanayochafua mazingira, iliyoanzishwa mwaka wa 2015 na Boris Johnson. Wahafidhina wanamshutumu kwa kutojali watu wa London wanaoteseka kutokana na hali ngumu ya maisha.

Mashambulizi haya wakati mwingine huvuka mipaka. Naibu Waziri Mkuu wa zamani wa Tories Lee Anderson alidai mnamo mwezi wa Februari 2024 kwamba wanamgambo wa Kiislam "wamechukua udhibiti" wa Sadiq Khan. "Alitoa mji wetu mkuu kwa washirika wake," amesema mbunge huyo ambaye leo alijiunga na chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Reform UK. Miaka michache mapema, mnamo mwaka 2019, Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump alimlenga Sadiq Khan wakati wa wimbi la mashambulio ya wanajihadi huko London, na kumwita "fedheha ya kitaifa" na "mtu aliyeshindwa kabisa". "Ni mmoja wetu tu ndiye aliyeshindwa, na sio mimi," Sadiq Khan alijibu.

Kikwazo kikubwa cha uchaguzi kwa wahafidhina

Zaidi ya kesi hii moja ya London, matokeo ya hivi punde zaidi ya uchaguzi wa serikali za mitaa yanathibitisha ushindi mkubwa wa chama cha Labour nchini humo, katika kura ya maoni katika mfumo wa mtihani wa mwisho kabla ya uchaguzi wa wabunge katika miezi michache. Kwa jumla, Labour ilishinda viti zaidi ya 180 na itaongoza mabaraza manane zaidi ya serikali za mitaa. Wahafidhina walipoteza zaidi ya viti 470 na kupoteza udhibiti wa angalau mabaraza kumi ya mitaa. Siku ya Ijumaa, matokeo ya kwanza yalionyesha kuwa Tories wangepata kushindwa kwao vibaya zaidi katika miaka arobaini katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Mbali na London, Labour katika hatua hii imeshinda chaguzi nane kati ya kumi na moja za manispaa ambazo zilifanyika katika miji mikubwa kadhaa nchini, kama vile Manchester, Liverpool, Leeds au Sheffield (South Yorkshire), lakini pia katika eneo la York na North Yorkshire, pale ambapo eneo la bunge la Waziri Mkuu liko. Yote si mazuri kwa Labor, hata hivyo, ambayo imepoteza wapiga kura kutokana na nafasi yake kuchukuliwa na baadhi ya wapiga kura wake kuwa inaunga mkono sana Israel katika mzozo kati ya Israel na Hamas huko Gaza.

Vyovyote vile, mafanikio makubwa ya upinzani wa chama cha Labour yanaimarisha matumaini yake kwamba kiongozi wake, Keir Starmer, atawasili katika mtaa wa Downing baada ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika baadaye mwaka huu. "Leo, tunasherehekea mwanzo wa ukurasa ambao unageuka, moja ya hatua za mwisho kabla ya uchaguzi wa wabunge", amesema  huko Mansfield huko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.