Pata taarifa kuu

Ufaransa kutuma wanajeshi Ukraine iwapo Kyiv itahitaji

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, kwenye mahojiano na Jarida la the Economist, amesema atakuwa tayari kutuma wanajeshi wa nchi yake nchini Ukraine, iwapo Kyiv itaomba msaada huo.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameongeza kuwa iwapo Urusi itashinda vita nchini Ukraine, hakutakuwa na usalama barani Ulaya, na tishio kwa mataifa ya EU na kusisitiza kuwa Ufaransa haiwezi kuruhusu hilo Urusi kushinda vita hivyo.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameongeza kuwa iwapo Urusi itashinda vita nchini Ukraine, hakutakuwa na usalama barani Ulaya, na tishio kwa mataifa ya EU na kusisitiza kuwa Ufaransa haiwezi kuruhusu hilo Urusi kushinda vita hivyo. REUTERS - Benoit Tessier
Matangazo ya kibiashara

Macron amesema iwapo vikosi vya Urusi vitaonekana kuilemea Ukraine na kuvuka mstari, ataidhinisha kutumwa kwa vikosi vya nchi yake, kumsaidia mshirika wake.

Kiongozi huyo wa Ufaransa ametoa kauli hii baada ya wiki iliyopita, kusema kuwa Ulaya inaweza kusambaratika na ipo kwenye hatari hiyo kufuatia hatua ya Urusi kuivamia Ukraine mwaka 2022.

Aidha, Macron kwenye mahojiano hayo yaliyochapishwa siku ya Alhamisi amesema chochote kinaweza kufanyika kwa sababu Urusi inayoweza kufanya chochote na hivyo Ulaya inapaswa kuwa tayari.

Ameongeza kuwa iwapo Urusi itashinda vita nchini Ukraine, hakutakuwa na usalama barani Ulaya, na tishio kwa mataifa ya EU na kusisitiza kuwa Ufaransa haiwezi kuruhusu hilo Urusi kushinda vita hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.