Pata taarifa kuu

Tafiti: Kirusi kipya cha Omicron hakina hatari kubwa kama kirusi cha Delta

Taasisi ya Kitaifa ya Magonjwa ya Kuambukiza nchini Afrika Kusini (NICD) siku ya Jumatano (Desemba 22) iliwasilisha ripoti ya utafiti wake, ambao bado haujathibitishwa na taasisi zingine, kuhusu ukali wa kirusi kipya cha Omicron, kilichogunduliwa na wanasayansi nchini humo, mwezi mmoja uliopita.

Mwanamke huyu akiwa akiandamana mtaani peke yake huko Johannesburg, Februari 8, 2021.
Mwanamke huyu akiwa akiandamana mtaani peke yake huko Johannesburg, Februari 8, 2021. REUTERS - SUMAYA HISHAM
Matangazo ya kibiashara

Uchambuzi wa kwanza unatoa hali ya matumaini kwa Afŕika Kusini, ambayo haimaanishi kuwa itakuwa hivyo katika sehemu nyingine za dunia. Tafiti zingine mbili za awali kutoka Uingereza, zimethibitisha utafiti wa Taasisi ya Kitaifa ya Magonjwa ya Kuambukiza nchini Afrika Kusini (NICD).

Wakati huo huo, utafiti mwingine nchini Afrika Kusini pia unaonyesha kuwa wimbi la Omicron ni dhaifu zaidi.

Unaonesha kuwa kulikuwa na uwezekano mdogo wa watu kuhitaji matibabu ya hospitali kwa asilimia 70 mpaka 80 ukilinganisha na mawimbi ya awali au aina nyingine za virusi vya corona .

Bado ni mapema kutoa picha kamili, lakini kulingana na mtaalam wa afya ya umma wa Taasisi hiyo, Wassila Jassat, data ya kwanza inatia moyo: "Wakati tunaona idadi ya kesi inazidi ile ya kirusi cha Delta, visa vya watu kulazwa hospitalini ni nusu ikilinganishwa na wakati wa mlipuko wa Delta, na idadi ya vifo imeongezeka kidogo sana ikilinganishwa na mlipuko wa awali. "

Ushahidi wa awali unaonesha kuwa watu wachache wanahitaji matibabu ya hospitali kuliko aina zingine ambapo makadirio yamepungua kati ya asilimia 30 hadi asilimia 70.

Lakini wasiwasi unabaki palepale hata kama wimbi hili si kali kwani hospitali zinaweza kuzidiwa na idadi kubwa ya watu wenye kesi za omicroni.

Kwa mara kwanza, zaidi ya kesi 100,000 zimeripotiwa nchini Uingereza ndani ya siku moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.