Pata taarifa kuu

Covid-19: Marekani yaidhinisha matumizi ya kidonge cha Pfizer

Siku mbili kabla ya Krismasi, kirusi kipya cha Omicronkinaendelea kusambaa kwa kasi nchini kote duniai, wakati Uingereza ikiripoti zaidi ya kesi 100,000 za maambukizi katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

Kulingana na majaribio ya kimatibabu, dawa hiyo inaweza kupunguza idadi ya watu kulazwa hospitalini na vifo kwa 88%, ameripoti mwandishi wetu wa Washington, Guillaume Naudin.
Kulingana na majaribio ya kimatibabu, dawa hiyo inaweza kupunguza idadi ya watu kulazwa hospitalini na vifo kwa 88%, ameripoti mwandishi wetu wa Washington, Guillaume Naudin. AP
Matangazo ya kibiashara

Rekodi ya kusikitisha kwa Uingereza: zaidi ya kesi 100,000 za Covid-19 zimerekodiwa katika muda wa saa 24. Kirusi kipya cha Omicron kimeendelea kuzua hofu na kuene kote duniani.

Jumatatu, Desemba 20, Waziri Mkuu wa Uingereza alikuwa ametangaza kutochukua vikwazo vipya, lakini akiweka uwezekano wa kufanya hivyo baadaye. Kwa sasa, serikali ya Johnson inaonekana kushindwa kukabiliana vilivo na kusambaa kwa kirusi hiki. Kwa sasa ulimwengu unaitazama Uingereza na unasubiri uchanganuzi wake juu ya aian hii mpya ya kirusi cha Omicron.

Kidonge cha Pfizer, Paxlovid, chaidhinishwa na mamlaka ya afya ya Marekani

Baada ya chanjo, matibabu ya kiubunifu: Maabara ya Pfizer yametengeneza kidonge kipya cha kutumiwa kwa watu walioambukizwa Covid-19. Jina lake: Paxlovid. Ni matibabu, yaliyotengwa kwa watu walio na zaidi ya umri wa miaka 12 walio katika hatari kubwa ya kukabiliwa vikali na ugonjwa huo. Inakuja kama mchanganyiko wa vidonge viwili vinavyotumiwa mara mbili kwa siku kwa kiîndi cha siku tano. Matumizi ya vidonge vya Paxlovid yanapaswa kuanza baada ya utambuzi na ndani ya siku tano baada ya dalili kujitokeza.

Kulingana na majaribio ya kimatibabu, dawa hiyo inaweza kupunguza idadi ya watu kulazwa hospitalini na vifo kwa 88%, ameripoti mwandishi wetu wa Washington, Guillaume Naudin.

Wakati huo huo Mkurungenzi Mkuu wa Shirika la Afya duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus anaonya kuwa hatua ya mataifa tajiri kuanza kutoa dozi ya tatu kwa raia wake, inaendeleza ubaguzi wa upatikanaji wa chanjo kwa mataifa masikini, hatua ambayo amesema haItasaidia kumaliza janga la Covid-19, hasa wakati huu kirusi cha Omicron kinapoendelea kusambaa duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.