Pata taarifa kuu

Ufaransa yaonya raia wake kuchukua tahadahari kuhusiana na kirusi cha Omicron

Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex, anaonya kuwa kirusi kipya cha Covid-19, Omicron kinasambaa kwa kasi sana barani Ulaya na kinatarajiwa kuwaambukiza watu wengi kuanzia mwaka ujao, huku uongozi wa jiji la Paris, ukifuta shamrashamra za kurusha fataki kuukaribisha mwaka mpya wa 2022.

Jean Castex alitangaza Jumatatu mlolongo wa hatua dhidi ya mlipuko wa 5 wa Covid-19 , ambayo inasambaa kwa kasi kubwa nchini Ufaransa.
Jean Castex alitangaza Jumatatu mlolongo wa hatua dhidi ya mlipuko wa 5 wa Covid-19 , ambayo inasambaa kwa kasi kubwa nchini Ufaransa. AFP - THOMAS SAMSON
Matangazo ya kibiashara

Onyo hili limekuja, baada ya Ufaransa kuanza kuzuia safari zisiso za lazima kwenda au kuingia nchini humo kutokea nchini Uingereza ambako kirusi cha Omicron kinasambaa kwa kasi.

Wakati huo huo Uingereza kufikia siku ya Ijumaa, ilikuwa imeripoti visa Elfu 15 vya Omicron pekee.

Mataifa mengine ya Ulaya ambayo yamechukua hatua kudhibiti kusambaa kwa kirusi hiki ni Ujerumani, Jamhuri ya Ireland na Uholanzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.