Pata taarifa kuu

Omicron: WHO yatoa wito wa kusitishwa kwa baadhi ya matukio ya msimu wa sikukuu

Shirika la afya duniani WHO linatoa wito kwa watu kuahirisha safari zao za likizo ili kusaidia katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Covid 19, wakati huu kirusi kipya cha Omicron kinapoendelea kusambaa kwa kasi duniani.

Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Desemba 20, 2021 huko Geneva, Uswisi.
Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Desemba 20, 2021 huko Geneva, Uswisi. AP - SALVATORE DI NOLFI
Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Tedros Ghebreyesus amesema kufutwa kwa baadhi ya matukio yaliyopangwa ni bora, kuliko kuondoa uhai na kuongeza kuwa maamuzi magumu ni lazima yakachukuliwa.

"Sisi wote tumechoshwa na janga hili, tungependa kuwa na familia zetu pamoja na marafiki, tunataka kurejea kwenye maisha yetu ya kawaida, njia ya haraka ya kufanikisha hili ni kwetu binafasi na viongozi kufanya maamuzi sahihi, ili kujilinda sisi na wengine, ni afadhali kuahirisha badala ya kupoteza kabisa, ni afadhali kuahirisha sasa, na kuherehekea baadaye, badala ya kusherehekea sasa hivi na kuomboleza baadaye, "  amesema Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Dunia, WHO.

Dokta Tedros amesisitiza pia janga hili linaweza kumalizika mwakani iwapo asilimia 70 ya watu katika kila nchi duniani watakuwa wamechanjwa ifikapo katikati ya mwaka huo 2022. amesisitiza pia janga hili linaweza kumalizika mwakani iwapo asilimia 70 ya watu katika kila nchi duniani watakuwa wamechanjwa ifikapo katikati ya mwaka huo 2022.

Wito huu umekuja, wakati huu mataifa kadhaa ya Ulaya kama Ufaransa, Ujerumani yakitangaza vikwazo vya kuingia katika nchi hizo ili kuepuka kusambaa kwa kirusi hiki, huku Uholanzi ikipiga marufuku watu kukutana siku ya Krismasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.