Pata taarifa kuu
WHO-COVID 19

WHO yaonya namna mataifa tajiri yanavyopambana na kirusi kipya cha Omicron

Mkurungenzi Mkuu wa Shirika la afya duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus anaonya kuwa hatua ya mataifa tajiri kuanza kutoa dozi ya tatu kwa raia wake, inaendeleza ubaguzi wa upatikanaji wa chanjo kwa mataifa masikini, hatua ambayo amesema hatasaidia kumaliza janga la Covid 19, hasa wakati huu kirusi cha omicron kinapoendelea kusambaa duniani.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus Fabrice COFFRINI AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Wakati hayo yakijiri, viongozi wa Ulaya wameanza kurejesha makataa za kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya Covid 19, wakati huu kirusi cha Omicron kikiendelea kusambaa kwa kasi kwenye bara hilo.

Nchi za Ujerumani na Ureno, ni miongoni mwa mataifa ambayo yametangaza makataa yatakayoanza kutekelezwa baada ya Krismas, huku raia wakitakiwa kutosongamana.

Hatua kama hizo zimetangazwa pia katika mataifa ya Finland na Uingereza, ambapo baadhi ya migahawa italazimika kufungwa mapema baada ya tarehe 24, huku raia nako wakitakiwa kuvaa barakoa na kupeana nafasi.

Hali kama hii inaripotiwa kwenye nchi za Sweden na Uholanzi, ambapo nchini Sweden migahawa michache imeruhusiwa kufanya kazi huku nchi ya Uholanzi yenyewe tayari ikitangaza sheria kali ikiwemo ya kutotembea kuanzia Jumatatu ya wiki hii.

Haya yanajiri wakati huu Ufaransa yenyewe ikianza kutoa chanjo dhidi ya virusi vya Corona kwa watoto kuanzia miaka 5 hadi 11, huku ikitarajiwa pia kutangaza makataa zaidi.

Watu milioni 1 na laki 5 wameripotiwa kufa barani Ulaya kutokana na Covid 19, huku wengine zaidi ya milioni 89 wakiwa wameambukizwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.