Pata taarifa kuu

Korea Kaskazini: Pyongyang yadai kuwa imeshinda Covid-19

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, anasema nchi yake imepata ushindi mkubwa dhidi ya Uviko-19, ambao ulionekana, kulingana na vyombo vya habari vya serikali, miezi mitatu iliyopita katika ardhi ya Korea Kaskazini. Pyongyang inadai kuwa hakuna "mgonjwa mpya" aliyeripotiwa tangu Julai 29 baada ya waginjwa 393,000 kugunduliwa na virusi vya Corona mnamo Mei 15.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akizungumza katika mkutano wa kitaifa wa mapitio ya kazi ya dharura ya kupambana na Uviko-19 huko Pyongyang mnamo Agosti 10, 2022.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akizungumza katika mkutano wa kitaifa wa mapitio ya kazi ya dharura ya kupambana na Uviko-19 huko Pyongyang mnamo Agosti 10, 2022. AFP - STR
Matangazo ya kibiashara

Wakati kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ametangaza ushindi wa kampeni ya kupambana na janga hilo katika mkutano wa kitaifa, dadake mdogo na naibu mkurugenzi wa idara ya Kamati Kuu ya Chama cha Wafanyakazi, Kim Yo-jong, anaishutumu Korea Kusini kwa kudondosha vipeperushi vilivyoambukizwa na coronavirus kuelekea Korea Kaskazini kwa kutumia baluni. Rejeleo la vipeperushi vilivyotumwa na makundi ya wapinzani wa Korea Kaskazini waishio Korea Kusini.

Kulingana na nakala iliyochapishwa asubuhi ya leo na Shirika la Habari la Korea Kaskazini (KCNA), limesema hasa kuwa Korea Kaskazini iko tayari kujibu "sio tu kwa kuangamiza virusi, lakini pia kwa kutokomeza mamlaka ya Korea Kusini." Tuhuma za vurugu ambazo ni sehemu ya vita vya maneno vinavyohuishwa mara kwa mara na nchi hizi mbili jirani zenye uhasama ili kuimarisha umoja wa ndani na, katika kesi hii, kujiondoa wajibu wowote katika kukabiliana na mgogoro unaohusishwa na Covid-19.

Kwa kufahamu kwamba Korea Kaskazini inaweza kutumia shutuma zake za mara kwa mara kama kisingizio cha uchochezi mpya wa kijeshi, Seoul imeshutumu "madai yasiyo na msingi" na kuthibitisha kuwa tayari kwa chochote kile kinachoweza kutokea".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.