Pata taarifa kuu

China: Watu 11 hawajulikani walipo baada ya mvua kubwa kunyesha kusini mwa nchi

Watu 11 wametoweka nchini China baada ya mvua kubwa iliyonyesha kusini mwa nchi hiyo ambayo imesababisha mafuriko na kusababisha makumi ya maelfu ya wakaazi kuhamishwa, vyombo vya habari vya serikali vimesema leo Jumatatu.

Mvua kubwa kusini mwa China sio kawaida haswa katika msimu wa joto.
Mvua kubwa kusini mwa China sio kawaida haswa katika msimu wa joto. © YUAN XIAOQIANG / IMAGINECHINA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangu siku ya Alhamisi, mvua kubwa imenyesha katika jimbo la Guangdong, ambalo ni tajiri zaidi na lenye watu wengi zaidi nchini na ambalo mji wake mkuu ni Canton na jimbo lenye viwanda vingi nchini China.

Mvua kubwa imesababisha mito kujaa kiasi kwamba kuna hofu ya kutokea kwa "mafuriko makubwa", kulingana na mamlaka.

"Jumla ya watu 11 hawajulikani walipo baada ya mvua kubwa kunyesha katika siku za hivi karibuni katika maeneo mengi ya Guangdong," shirika la habari la Xinhua limesema, likinukuu chombo kinachosimamia hali za dharura.

Hali mbaya ya hewa katika siku za hivi karibuni ilisababisha maporomoko ya ardhi katika maeneo ya milimani.
Hali mbaya ya hewa katika siku za hivi karibuni ilisababisha maporomoko ya ardhi katika maeneo ya milimani. REUTERS/Jason Lee

Zaidi ya watu 53,000 katika jimbo hilo walilazimika kuhamishwa, Xinhua imesema.

Wengi wao walihamishwa kutoka Qingyuan, mji ulioko yapata kilomita sitini kutoka Guangzhou na kuvuka na Mto Bei, kijito cha Delta ya Mto Pearl.

Mvua kubwa inayoambatana na ngurumo na upepo mkali kulingana na mamlaka ya hali ya hewa ya China inatarajiwa kunyesha siku ya Jumatatu katika mji mkuu wa Shenzhen, unaopakana na Hong Kong na makao makuu ya makampuni mengi ya teknolojia.

Hali mbaya ya hewa katika siku za hivi karibuni ilisababisha maporomoko ya ardhi katika maeneo ya milimani.

Watu sita walijeruhiwa na wengine kadhaa kukwama karibu na mji wa Jiangwan kaskazini mwa Guangdong, kulingana na televisheni ya serikali CCTV.

Picha zinazorushwa hewani na kituo hicho zinaonyesha nyumba kwenye kingo za mto zilizoharibiwa na tope nyingi, na watu wakihudumiwa na idara ya huduma za dharura kwenye uwanja wa michezo uliojaa maji.

Mvua kubwa kusini mwa China sio kawaida haswa katika msimu wa joto.

Lakini nchi hiyo imekabiliwa na hali mbaya ya hewa katika miezi ya hivi karibuni, ikichochewa na mabadiliko ya tabianchi kulingana na wanasayansi.

Mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa na gesi chafuzi zinazotolewa na binadamu yanafanya matukio ya hali mbaya ya hewa kuwa ya mara kwa mara na makali zaidi, wanasayansi wanasema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.