Pata taarifa kuu
IMANI-UTAPELI

Kenya: Polisi yamsaka mchungaji kwa ulaghai mkubwa baada ya kutapeli watu

Nchini Kenya, kunaripotiwa kashfa mpya inayomhusisha mchungaji James Wanjohi. Mchungaji huyu ndiye mwanzilishi wa Church of Jesus Culture Ministries, Nairobi. Tangu Ijumaa, amepigwa marufuku kuondoka nchini. Anashukiwa kuwa amefuja shilingi milioni 600, au zaidi ya euro milioni 4.

Ukurasa wa Facebook wa mchungaji wa Kenya James Wanjohi.
Ukurasa wa Facebook wa mchungaji wa Kenya James Wanjohi. © capture d'écran Facebook
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Nairobi, Gaëlle Laleix

Katika mahubiri yake kwenye YouTube, James Wanjohi anajionyesha kama "self made man ", mtu ambaye alianza bila chochote na kufaulu kwa kutumia njia alizojitengenezea peke yake. Kwa sababu James Wanjohi sio tu mchungaji, pia ana shirika la usafiri, kituo cha mafunzo cha barrista na shirika la ushauri wa uhamiaji.

Kwa shilingi 100,000 hadi 140,000, au euro 700 hadi 950, James Wanjohi hutoa visa za kwenda Canada, Marekani, Uingereza au Australia na kupata kazi ya uhakika. Utaratibu wote hufanywa ndani ya kipindi cha miezi mitatu.

Mamia ya watu walidanganywa kwa njia hii. Kulingana na polisi ya Kenya, wengi wa waathiriwa walisajiliwa kupitia Kanisa la James Wanjohi. Ulaghai huo uliendelea hivi kwa miezi mingi, hadi, bila habari za matendo yao, baadhi ya waathiriwa waliwatahadharisha polisi. Leo, wakurugenzi wa kampuni za James Wanjohi wametiwa mbaroni lakini mchungaji huyo hajapatikana.

Kesi hii inaibua upya mjadala kuhusu udhibiti wa dini nchini Kenya. Baada ya mauaji ya Shakahola, mwezi wa Aprili 2023, tume ya bunge la seneta iliundwa ili kutathmini ushauri wa sheria mpya lakini ikakumbana na kizuizi kutoka kwa viongozi wa kidini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.