Pata taarifa kuu
USALAMA-UCHUNGUZI

Mahakama ya Kenya yatishia kumwachilia mchungaji anayeshtakiwa kwa mauaji ya Shakahola

Mahakama ya Kenya siku yaJumanne imeipa mamlaka siku 14 kuanzisha kesi dhidi ya Paul Nthenge Mackenzie, chini ya adhabu ya kumwachilia mchungaji huyo aliyezuiliwa tangu mwezi Aprili mwaka uliyopita katika uchunguzi wa vifo vya waumini 429 wa dhehebu lake la kiinjilisti.

Dereva wa teksi kabla ya kujitangaza kuwa mchungaji, Paul Nthenge Mackenzie amekuwa kizuizini tangu Aprili 14, siku moja baada ya kupatikana kwa waathiriwa katika msitu wa Shakahola.
Dereva wa teksi kabla ya kujitangaza kuwa mchungaji, Paul Nthenge Mackenzie amekuwa kizuizini tangu Aprili 14, siku moja baada ya kupatikana kwa waathiriwa katika msitu wa Shakahola. © capture AFPTV
Matangazo ya kibiashara

Kuzuiliwa kwa Paul Nthenge Mackenzie kuliongezwa mara kadhaa ili kuruhusu msako wa wahanga katika msitu wa Shakahola (kusini-mashariki), ambapo "Kanisa lake la Kimataifa la Habari Njema" lilikutana, ambalo aliwahubiria kufunga hadi kifo. ” kabla ya mwisho wa dunia mnamo mwezi Agosti 2023. Ikiitwa “mauaji ya Shakahola”, kashfa hii imezua hofu na sintofahamu nchini Kenya, nchi yenye Wakristo wengi yenye “makanisa” rasmi 4,000.

Ikitoa uamuzi kuhusu ombi la kuendelea kuzuiliwa kwa siku 180 lililotolewa mwezi Septemba na waendesha mashtaka, mahakama katika mji wa pwani wa Mombasa imebainisha siku ya Jumanne kuwa Mchungaji Mackenzie na washtakiwa wenzake 29 tayari walikuwa wametumikia siku 117, "muda wa kutosha kwa uchunguzi unaoendelea kuweza kukamilika. ".

Ikikumbusha kwamba "hiki ndicho kizuizi kirefu zaidi kabla ya kesi katika historia ya nchi" tangu kutangazwa kwa katiba yake mnamo mwaka 2010, mahakama ilitoa siku 14 za ziada. "Iwapo hakuna uamuzi wa kuwashtaki (watuhumiwa) utakuwa umechukuliwa baada ya muda huu kuisha, mahakama itazingatia kuwaachilia kwa masharti yatakayoamuliwa na mahakama," ameandika Jaji Yusuf Abdallah Shikanda katika uamuzi wake.

Waendesha mashitaka walitangaza mwezi Mei kwamba wataleta mashtaka ya "ugaidi" dhidi ya mtuhumiwa wa mauaji ya Shakahola. Dereva wa teksi kabla ya kujitangaza kuwa mchungaji, Paul Nthenge Mackenzie amekuwa kizuizini tangu Aprili 14, siku moja baada ya kupatikana kwa waathiriwa wa kwanza katika msitu wa Shakahola. Tangu wakati huo, miili 429 ilipatikana katika eneo hili la "kichaka" la pwani ya Kenya.

Uchunguzi wa upasuaji wa maiti ulifichua kuwa wengi wa waathiriwa walikufa kwa njaa, pengine baada ya kufuata mahubiri ya Paul Nthenge Mackenzie. Baadhi, kutia ndani watoto, walinyongwa, kupigwa au kuzidiwa.

Watu kumi na sita wanatuhumiwa kuwa sehemu ya kundi la "wachungaji" wa pasta waliohusika na kuhakikisha kuwa hakuna muumini aliyefungua mfungo au kutoroka msituni. Mamalaka ilishutumiwa vikali kwa kutozuia vitendo vya Mchungaji Mackenzie, aliyekamatwa mara kadhaa kwa kuhubiri kwake kupita kiasi.

Mnamo mwezi Machi, aliachiliwa kwa dhamana licha ya mashtaka dhidi yake baada ya vifo vya watoto wawili, ambao walikufa kwa njaa katika uangalizi wa wazazi wao wanaohusishwa na dhehebu hilo. Tume ya Seneti ilitaja "mapungufu" katika mfumo wa mahakama na polisi, katika ripoti iliyochapishwa mwezi Oktoba mwaka jana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.