Pata taarifa kuu
Jua Haki Zako

Kenya : Serikali yaanza kutoa miili ya waumini waliofariki baada ya kususia chakula ili wamuone Yesu

Imechapishwa:

 Unamkumbuka  kiongozi wa wa dini Paul Mackenzi anayetuhumiwa kwa kushiwishi waumini wake kususia chakula hadi kufa, ili kukutana na yesu nchini Kenya.


Mchungaji  mwenye utata Paul Nthenge Mackenzie (kushoto) akitembea akiwa amezungukwa na Maafisa wa Polisi wa Kenya na washtakiwa wengine alipokuwa akifikishwa katika Mahakama ya Shanzu mjini Mombasa Januari 18, 2024. Mahakama ya Kenya mnamo Januari 18, 2024 ilimfungulia 
Kiongozi huyo wa dini mashtaka ya  ugaidi pamoja na vifo vya wafuasi wake zaidi ya 400. Paul Nthenge Mackenzie anadaiwa kuwachochea washirika wake kufa njaa ili "kukutana na Yesu" kisa kilichoshangaza ulimwengu. (Picha na AFP)
Mchungaji mwenye utata Paul Nthenge Mackenzie (kushoto) akitembea akiwa amezungukwa na Maafisa wa Polisi wa Kenya na washtakiwa wengine alipokuwa akifikishwa katika Mahakama ya Shanzu mjini Mombasa Januari 18, 2024. Mahakama ya Kenya mnamo Januari 18, 2024 ilimfungulia Kiongozi huyo wa dini mashtaka ya ugaidi pamoja na vifo vya wafuasi wake zaidi ya 400. Paul Nthenge Mackenzie anadaiwa kuwachochea washirika wake kufa njaa ili "kukutana na Yesu" kisa kilichoshangaza ulimwengu. (Picha na AFP) AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Baada ya takriban  mwaka moja na mwezi mmoja wa serikali ya Kenya kufukua miili ya waumini   waliofariki na kuzikwa katika msiku wa Shakahola na kuzifanyia uchuguzi wa vina saba yaani DNA, serikali sasa imeanza kutoa miili hiyo kwa familia za jamaa waliofariki.

Serikali ya Kenya kupitia kwa mwanapatholijia wake mkuu daktari Johason Odour, imesema ilichukuwa muda mrefu kutoa miili kwa family zilizoathirika kutokana na kuharibika kupita kiasi.

Soma piaWazee wauliwa pwani ya Kenya kwa tuhuma za kwamba ni wachawi

Katika haya  mwanahabari Diana Wanyonyi kutoka pwani ya Kenya  alihudhuria mazishi ya baadhi ya waathiriwa wa mafunzo ya itikadi kali Paul Mackenzie na anasimulia hali ilivyokuwa 

Vipindi vingine
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.