Pata taarifa kuu

Kenya: Baada ya mafuriko, tishio la kipindupindu latanda katika vitongoji duni vya Nairobi

Mvua kubwa na mafuriko vinaendelea nchini Kenya. Hali hiyo tayari imesababisha waathiriwa 228. Wikiendi hii, mamlaka iliwahamisha raia, wakati mwingine kwa nguvu, wanaoishi katika maeneo ya mafuriko. Hii ilikuwa hasa katika vitongoji duni vya Nairobi. Lakini leo, watu hawa wanakabiliana na shida nyingine: kuenea kwa magonjwa. Ripoti kutoka Kibera, makazi duni makubwa zaidi katika mji mkuu.

Mfanyakazi wa shirika la Msalaba Mwekundu katika barabara iliyofurika maji katika wilaya ya Kitengela, karibu na Nairobi, Mei 1, 2024.
Mfanyakazi wa shirika la Msalaba Mwekundu katika barabara iliyofurika maji katika wilaya ya Kitengela, karibu na Nairobi, Mei 1, 2024. REUTERS - Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu maalum huko Kibera, Gaëlle Laleix

Katika zahanati ya Shofco, katika wilaya ya Makina huko Kibera, Bahati anamkumbati mtoto wake. Mafuriko yalisomba sehemu ya nyumba yake. Pamoja na hayo, Bahati bado anaishi katika kijiji hiki kwa sababu hana pa kwenda. Kwa siku kadhaa, mtoto wake amekuwa akiugua sana: “Ana ana maumivu y kifua na amekuwa akikohoa kwa siku nne sasa. Hapo awali, mtoto wangu alikuwa sawa, lakini tangu mvua ilianza kunyesha, mapafu yake yameziba. Wafanyakazi wa kijamii waliniagiza nije hapa. Nina wasiwasi sana. "

Wellington amepoteza kila kitu. Kwa nyumba yake, kuta tu ndio zimesalia ... na leo ana wasiwasi kuhusu afya yake: "Nilikuwa mbele ya nyumba yangu nikifikiria siku yangu itakuwaje nilipopigwa na maumivu ya tumbo na na kuharisha. Wakati mvua na mafuriko zilipoanza ndipo nilianza kupata homa. "

Kuhara, homa, kikohozi ... dalili ziko tofauti, lakini sababu ni moja: maji machafu ambayo tangu mafuriko yamekuwa kila mahali. Wagonjwa 34 wa kipindupindu wamerekodiwa na Wizara ya Afya, haswa katika Kaunti ya Tana River, mashariki mwa nchi. Katika vitongoji duni vya Nairobi, ambako magonjwa haya ya milipuko yanatokea mara kwa mara, wasiwasi unaongezeka "Maji hayashughulikiwi inavyopaswa kuwa," anaelezea Dk. Dalmas Otieno, daktari katika zahanati ya Shofco. Mara nyingi utakuta milingoti iko wazi. Pamoja na mafuriko, maji machafu yalipenya ndani ya milingoti hiyo. Tunafanya kazi na wahudumu wa afya ya jamii ambao wamepewa zinki ili waweze kusambaza, chumvi za kurejesha maji na Aquatab kuuwa wadudu na minyoo kwenye maji. "

Huko Kisumu Ndogo, wilaya nyingine ya Kibera, Nicolas anaishi karibu na Mto Nairobi. Ijapokuwa nyumba yake ilijaa maji, aliamua kubaki humo licha ya hali mbaya ya usafi: “Hatuna bafu na ni vigumu kupata maji. Kuna mto huko, tunaenda kuchukua maji ambayo tunatumia kwa kuoga, lakini maji haya sio ya binadamu. Hatuna pesa, hatuna kazi, hatuwezi kununua maji, ni ghali. "

Dumu la lita 20 ya maji huko Kibera linagharimu shilingi 20 (karibu senti 14 za euro). Wellington anaishi Lindi. Anapendelea kutumia vyoo vya mitaani: “Vyoo hivi ni vya umma, havitoshi, maji hakuna. Vyoo hivi ni vichafu sana kwa sababu hakuna mtu anayevishughulikia kwa usafi. Kila mtu anakuja, anavitumia na kuondoka. Mara nikienda huko, natumia maji ya bomba za barabarani, maji hayo ndio tunatumia kwa kuoga. "

Kwa mujuibu wa Dk Dalmas Otieno, tuna wasiwasi kutokea kwa mlipuko wa janga la kipindupindu: "Vitongoji duni vyote viko hatarini, kwa sababu maji machafu huvamia maeneo yote ambayo mifereji ya maji ni duni. Mlipuko wa Kipindupindu unaweza kuwa hatari sana hapa. Kwa hiyo moja ya mambo tunayojaribu kufanya ni kuwafundisha watu jinsi ya kushughulikia usafi wa maji na kushughulikia magonjwa ya kuhara mapema. "

Katika taarifa yake ya hivi punde iliyochapishwa leo, mamlaka ya Hali ya Hewa ya Kenya inatabiri mvua kubwa zaidi kwa wiki nzima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.