Pata taarifa kuu

Kenya: Ni wiki moja sasa tangu mafuriko kuwaathiri wakaazi wa Mai Mahiu

Nchini Kenya, wiki moja baada ya watu zaidi ya 50 kupoteza maisha katika eneo la Mai Mahiu, Kaunti ya Nakuru, ambapo makaazi yalisombwa na mafuriko, baada ya kupasuka kwa kingo za bwawa lakuhifadhia maji, Hali ya manusura kwenye eneo hilo ni mbaya, ambapo wanaishi kwa kutegemea msaada wa serikali na wahisani.

Zaidi ya watu 50 walithibitishwa kufariki katika mkasa huo kwenye kijiji cha Kamuchiri mjini Mai Mahiu katika mkoa wa bonde la ufa nchini Kenya. Tarehe 30 Aprili 2024.
Zaidi ya watu 50 walithibitishwa kufariki katika mkasa huo kwenye kijiji cha Kamuchiri mjini Mai Mahiu katika mkoa wa bonde la ufa nchini Kenya. Tarehe 30 Aprili 2024. © Brian Inganga / AP
Matangazo ya kibiashara

Jumapili ya tarehe tano mwezi huu, wakaazi wa vijiji vitano katika eneo la Mai Mahiu, walienda kulala kama kawaida, lakini ilipofika Alfajiri, wengine walikuwa wameangamia kwa maji.

Elizabeth Njeri ambaye amezaliwa katika mojawapo ya kijiji katika mji Mai Mahiu, anaeleza alivyowapoteza wapendwa wake.

‘‘Watu waliofariki katika huu mkasa tumeishi nao tangu mwaka wa 1970.’’ alisema Elizabeth Njeri, Mkaazi wa Mai Mahiu.

00:16

Elizabeth Njeri, Mkaazi wa Mai Mahiu

Hofu inaonekana kwenye nyuso za walionusurika. Wanaonekana kukata tamaa baada ya janga hilo.

“Hapa hali yetu ya kisaikolojia sio sawa kabisa maana mvua ikiendelea kunyesha tunakuwa na wasiwasi.” Alieleza Geofrey Wainana makaazi wa eneo kulikotokea mkasa.

00:10

Alieleza Geofrey Wainana makaazi wa eneo kulikotokea mkasa

Wakati wa janga hilo, Stephene Macharia anakumbuka kuwaokoa wapendwa wake, lakini maji yalimzidi akaamua kujiokoa.

“Mimi baada ya kuwaokoa watu wangu nilipanda juu ya choo na nilikuwa naangalia tu maji yakipita nikiwa juu ya choo.” Alisema Macharia mmoja wa waathiriwa wa mafuriko.

00:15

Macharia ni mmoja wa walioathirika na mafuriko hayo

Alice Njoki anasema kuponea kwake, ni kwa sababu hakuwepo nyumbani usiku huo.

“Mimi hata watu wa kwetu wameshangaa sana kuniona maanda wengi walidhani pia nami nimesombwa na maji.” alisema Alice Njoki.

00:16

Alice Njoki, Aliyenusurika mafuriko

Soma piaIdadi ya waliofariki katika mafuriko nchini Kenya imefikia 228

Hadi sasa kuna wale ambao hawajawapata wapendwa wao huku walionusurika wakiwa katika shule ya Sekondari ya Ngeya, maisha yao yamebadilika, wapendwa wao wamepoteza maisha, na makaazi yao hayapo tena.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.