Pata taarifa kuu

Shule nchini Kenya kufunguliwa Jumatatu ya wiki ijayo: Rais Ruto

Rais wa Kenya William Ruto ameagiza shule zote zifunguliwe Jumatatu ya wiki ijayo baada ya kufungwa awali kutokana na mafuriko yaliokuwa yanashuhudiwa katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Tarehe ya shule kufunguliwa ilisongezwa mbele kutokana na athari za mafuriko nchini Kenya.
Tarehe ya shule kufunguliwa ilisongezwa mbele kutokana na athari za mafuriko nchini Kenya. © State House Kenya
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa rais Ruto, uamuzi huo umeafikiwa baada ya mashauriano ya kina na idara ya hali ya hewa ambayo imethibitisha kwamba mvua itapungua katika siku zijazo.

Shule katika taifa hilo la Afrika Mashariki zilitarajiwa kufunguliwa tarehe 29 ya mwezi uliopita lakini wizara ya elimu ikasongeza mbele tarehe hiyo kutokana na athari za mafuriko.

 “Wazazi wote wanaelekezwa kwa mujibu wa ushauri wa idara ya hali ya hewa na tathmini ya serikali ya Kenya kuwa shule zitafunguliwa Jumatatu ya wiki ijayo na wazazi wawaandae wanao kwenda shuleni.” Alisema rais Ruto.

Aidha rais ameeleza kuwa serikali yake itatoa pesa kwa ajili ya ukarabati wa shule ambazo zimeharibiwa kutokana na mafuriko.

Kando na suala la shule kufunguliwa wiki ijayo rais Ruto pia amewataka raia nchini humo kutumia siku ya Ijumaa ya wiki hii kupanda miche kwa ajili ya kuwakumbuka wahanga wa mafuriko.

Maeneo tofauti nchini Kenya yamekuwa yakikabiliwa na mafuriko katika kipindi cha wiki kadhaa zilizopita, vifo na uharibifu vikiripotiwa.
Maeneo tofauti nchini Kenya yamekuwa yakikabiliwa na mafuriko katika kipindi cha wiki kadhaa zilizopita, vifo na uharibifu vikiripotiwa. REUTERS - Thomas Mukoya

Raia wa Kenya wametakiwa kutumia siku hiyo ambayo itakuwa likizo ya kitaifa kupanda angalau miche 50, serikali yake ikilenga kupanda miche milioni 200.

Kuhusu suala la miundo mbinu ilioharibiwa na na mafuriko, rais Ruto ameeleza kuwa serikali yake itashirikiana na washirika wake kukarabati barabara zilizoharibika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.