Pata taarifa kuu

London na Kigali zatia saini mkataba mpya wa uhamiaji

Wiki tatu baada ya kukataliwa kwa mradi wa awali, London na Kigali zimetia saini mkataba mpya nchini Rwanda siku ya Jumanne unaolenga kufufua makubaliano yenye utata ya kuwafukuza wahamiaji waliowasili nchini Uingereza kinyume cha sheria nchini humo.

Upande wa kushoto, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza James Cleverly akipeana mkono na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Vincent Biruta baada ya kusainiwa kwa mkataba mpya wenye utata mjini Kigali Jumanne, Desemba 5, unaolenga kuwafukuza wahamiaji waliowasili kinyume cha sheria nchini Uingereza kwenda Rwanda.
Upande wa kushoto, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza James Cleverly akipeana mkono na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Vincent Biruta baada ya kusainiwa kwa mkataba mpya wenye utata mjini Kigali Jumanne, Desemba 5, unaolenga kuwafukuza wahamiaji waliowasili kinyume cha sheria nchini Uingereza kwenda Rwanda. via REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Uingereza inajaribu kuokoa hatua hii kuu ya sera yake dhidi ya uhamiaji haramu, baada ya kashfa iliyotolewa katikati ya mwezi Novemba na Mahakama ya Juu ya Uingereza ambayo ilithibitisha kuwa mradi wake haukuwa halali kama ilivyo. Mkataba huo mpya umetiwa saini katika mji mkuu wa Rwanda Kigali na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza James Cleverly na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Vincent Biruta.

"Tumeendeleza ushirikiano huu na Uingereza kwa sababu tunaamini kwamba tuna jukumu la kutekeleza katika mgogoro huu wa uhamiaji haramu," Vincent Biruta amehakikisha wakati wa mkutano na waandishi wa habari, wakati James Cleverly alipotangaza "kuipongeza sana serikali ya Rwanda, ambayo ilikosolewa sana.”

Mkataba huu mpya "utajibu wasiwasi wa Mahakama ya Juu kwa kuhakikisha hasa kwamba Rwanda haitawafukuza katika nchi nyingine watu waliohamishwa ndani ya mfumo wa ushirikiano", ulihakikishiwa mapema kidogo katika taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, kwa kujibu moja ya hoja kuu za mahakimu.

Baada ya uamuzi wa Mahakama ya Juu, James Cleverly alihakikisha kwamba "mkataba wa kisheria" utatiwa saini na Kigali ili kutoa dhamana juu ya hatima ya wahamiaji waliofukuzwa kutoka Uingereza. Mara baada ya kusainiwa, andiko hili lazima liidhinishwe na Mabunge ya Uingereza na Rwanda.

"Nchi salama"

Kabla ya kutia saini makubaliano hayo, mkuu mpya wa Ofisi ya Mambo ya Ndani ametembelea eneo la kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya Rwanda. "Ni wazi kwamba Rwanda ni nchi salama, na tunafanya kazi kwa kasi endelevu ili kuendeleza ushirikiano huu ili kusitisha boti (zinazovuka mto na bahari) na kuokoa maisha ya watu," amesema James Cleverly, akinukuliwa katika taarifa hii.

Mnamo Novemba 15, majaji wakuu wa Uingereza walikataa rufaa kutoka kwa serikali ya Rishi Sunak na waliamua kwamba Mahakama ya Rufaa ilikuwa sahihi kuhitimisha kwamba Rwanda haiwezi kuchukuliwa kuwa nchi ya tatu salama.

Mara tu baada ya uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Uingereza, Kigali ilitangaza "kupinga uamuzi kwamba Rwanda si nchi ya tatu salama kwa wanaotafuta hifadhi na wakimbizi." Rwanda inatawaliwa kwa mkono wa chuma tangu mwaka 1994 na Paul Kagame.

"Imezuiwa"

Tangu kuanza kwa mwaka huu, watu 29,705 wamevuka bahari kwa kutumia boti ndogo, kulingana na hesabu ya shirika la habari la AFP. "Sijafurahia kuona sera yetu na Rwanda inazuiwa," Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak alisema katika mahojiano Jumatatu jioni na Gazeti la The Sun. Mbali na mkataba huo, serikali ya Uingereza itaanzisha "sheria ya dharura" katika Bunge ili kutaja Rwanda kama nchi salama na hivyo "kukomesha hali hii ya yenye utata", alisema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.