Pata taarifa kuu

Kenya : Wakimbizi zaidi ya elfu 20 wameathiriwa na mafuriko : UNHCR

Shirika la wakimbizi duniani, UNHCR nchini Kenya, limesema zaidi ya wakimbizi elfu 20 wameachwa bila makao baada ya nyumba zao kuharibiwa na mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini humo kwenye kambi kubwa ya Dadaab.

Wakimbiizi katika kambi ya Kakuma kaskazini mashariki mwa Kenya pia wameathiriwa na mafuriko.
Wakimbiizi katika kambi ya Kakuma kaskazini mashariki mwa Kenya pia wameathiriwa na mafuriko. © UNHCR KENYA
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa fupi shirika hilo limetangaza kuwa sasa wakimbizi hao elfu-ishirini wanaishi kwenye madarasa ya shule saba mbali na sehemu ilioyokumbwa na mafuriko ambako vyoo vimefurika maji na kuna hatari ya kutokea magonjwa yanayosababishwa na maji machafu.

Korad Abdiwanhab, anayeongea Kisomali, ni mmoja ya wakimbizi waliolazimishwa kuhama walipokuwa wanaishi kutokana na mafuriko.

‘‘Maji yaliingia kwenye nyumba kutoka pande zote mashariki, magharibi, kusini na kaskazini. Mara tu nilipoona maji yameingia niliamka ghafla na kumwamsha mtoto wangu mlemavu na watoto wengine.’’ alisema Korad Abdiwanhab.

00:27

Korad Abdiwanhab, Mmoja wa wakimbizi

Mohamed Aden Maalim, afisa wa shirika la wakimbizi Dadaab anaeleza kwa  hali ilivyo Dadaab kwa sasa.

‘‘Tumekabiliwa na mvua kubwa ambayo imesababisha mafuriko kwenye kambi za wakimbizi, mashirika mbalimbali ya wakimbizi yameungana kwa pamoja kuwasaidia walioathirika.’’ alieleza Mohamed Aden Maalim, afisa wa shirika la wakimbizi Dadaab.

00:24

Mohamed Aden Maalim, afisa wa shirika la wakimbizi Dadab

Katika eneo la Dadaab kuna kambi tatu za wakimbizi ambazo ni makao ya wakimbizi elfu-mia-mbili-arobaini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.