Pata taarifa kuu

Kufukuzwa kwa wanaotafuta hifadhi nchini Rwanda: Kigali 'yapinga' uamuzi wa Uingereza

Kigali "inapinga" uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Uingereza kuthibitisha Jumatano uharamu wa mpango wa serikali wenye utata wa kuwafukuza waomba hifadhi nchini Uingereza na kuwapeleka nchini Rwanda, msemaji wa serikali ya Rwanda ameliambia shirika la habari la AFP.

Boris Johnson akipeana mkono na Paul Kagame kabla ya mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi za Jumuiya ya Madola mjini Kigali, Rwanda, Juni 23, 2002.
Boris Johnson akipeana mkono na Paul Kagame kabla ya mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi za Jumuiya ya Madola mjini Kigali, Rwanda, Juni 23, 2002. AP - Dan Kitwood
Matangazo ya kibiashara

"Hatimaye huu ni uamuzi wa mfumo wa mahakama ya Uingereza. Hata hivyo, tunapinga uamuzi kwamba Rwanda si nchi ya tatu salama kwa wanaotafuta hifadhi na wakimbizi," amesema Yolande Makolo.

Majaji wakuu wa Uingereza walikataa rufaa kutoka kwa serikali ya Rishi Sunak na waliamua kwamba Mahakama ya Rufaa ilikuwa sahihi kuhitimisha kwamba Rwanda kwama haiwezi kuchukuliwa kuwa nchi ya tatu salama.

Kwa upande wa haki za binadamu, Rwanda inatajwa mara kwa mara kwa ukandamizaji mkali wa upinzani wa kisiasa na kushindwa kwake kuheshimu uhuru wa kujieleza. "Tunachukua majukumu yetu ya kibinadamu kwa uzito na tutaendelea kuyatimiza," amesema Yolande Makolo.

Mradi huo ulitangazwa mwaka mmoja na nusu uliopita, wakati huo chini ya serikali ya Boris Johnson. Mkataba huu, ambao unaendelea kwa kipindi cha miaka mitano, ulitaka London kuilipa Kigali pauni milioni 140 (euro milioni 160), pesa zilizotengwa kwa msaada wa maendeleo na utunzaji wa wahamiaji katika nchi hii ya Afrika.

Katikati ya mwaka 2022, safari ya kwanza ya ndege ilisitishwa baada ya uamuzi wa Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu (ECHR). Kisha mwishoni mwa mwezi Juni mwaka jana, Mahakama ya Rufaa ya London iliamua mradi huo kuwa "ni kinyume cha sheria", ikigundua kuwa Rwanda haiwezi kuchukuliwa kama "nchi ya tatu salama".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.