Pata taarifa kuu

Kigali yapongeza uamuzi wa mahakama ya London kuhusu wahamiaji haramu

Rwanda imekaribisha uamuzi wa Mahakama  Kuu jijini London, iliyoamua hapo jana, kuwa mpango wa serikali ya Uingereza kuwahamishia wahamiaji haramu katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki ni halali kisheria.

Boris Johnson akipeana mkono na Paul Kagame kabla ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola mjini Kigali, Rwanda, Juni 23, 2002.
Boris Johnson akipeana mkono na Paul Kagame kabla ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola mjini Kigali, Rwanda, Juni 23, 2002. AP - Dan Kitwood
Matangazo ya kibiashara

Naibu msemaji wa serikali ya Rwanda, Alain Mukuralinda amesema, Kigali ipo tayari kuwapokea wahamiaji hao, ili waanze maisha mapya katika taifa hilo. 

Licha ya uamuzi huo wa Mahakama, wanaharakati wa haki za binadamu, wameapa kukataa rufaa, kuizuia serikali ya Uingereza kutekeleza mpango huo, wanaosema ni kinyume cha haki za binadamu. 

Hata hivyo, Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak amekaribisha uamuzi wa Uingereza na kueleza mpango huo unalenga kupambana na ongezeko la wahamiaji haramu nchini humo. 

Mwezi Juni, Mahakama ya Haki za binadamu ya Umoja wa Ulaya, ilisitisha mpango wa kuanza kuwasafirisha wahamiaji hao nchini Rwanda, baada ya wanaharakati kudai kuwa nchi hiyo sio salama kwa watu hao, madai ambayo Kigali inakanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.