Pata taarifa kuu

Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola wafunguliwa mjini Kigali

Ijumaa hii, Juni 24, wawakilishi wa nchi za Jumuiya ya Madola wanakutana mjini Kigali. Ni ufunguzi rasmi asubuhi ya leo wa mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa jumuiya hii inaojumuisha nchi 54, zikiwemo 19 kutoka Afrika. Huu ni mkutano wa kwanza wa aina hiyo ndani ya kipinci cha miaka minne.

Boris Johnson akipeana mkono na Paul Kagame kabla ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola mjini Kigali, Rwanda, Juni 23, 2002.
Boris Johnson akipeana mkono na Paul Kagame kabla ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola mjini Kigali, Rwanda, Juni 23, 2002. AP - Dan Kitwood
Matangazo ya kibiashara

Hafla hiyo iliahirishwa mara mbili kwa sababu ya janga la Covid-19 na marais wengi na mawaziri wakuu wanahudhuria.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson aliwasili Kigali Alhamisi Juni 23 na alikuwa mwepesi kutetea ushirikiano wake wa ushirikiano katika masuala ya uhamiaji na Rwanda, mpango uliolaaniwa na Umoja wa Mataifa na mashirika ya haki za binadamu. "Ukosoaji unapewa nafasi na ni haki kwa mkosioaji," waziri mkuu wa Uingereza aliwaambia waandishi wa habari baada ya kuzuru shule moja mjini Kigali. Boris Johnson pia alizungumzia suala hilo wakati wa mahojiano ya moja kwa moja na Rais Paul Kagame.

Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, Amir wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, Rais wa Uganda Yoweri Museveni na Muhammadu Buhari wa Nigeria pia wapo mjini Kigali.

Katika ajenda kuna mazungumzo yatakayofanyika farghani kuhusu maendeleo endelevu na kufufua uchumi wa nchi za Jumuiya ya Madola baada ya mgogoro wa kiafya wa uliosababishwa na Corona na katika muktadha wa vita vya Ukraine, mazungumzo yaliyoandaliwa jana na mkutano wa mawaziri Mambo ya nje wa nchi za Jumuiya ya Madola.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.