Pata taarifa kuu

Idadi ya waliofariki katika mafuriko nchini Kenya imefikia 228

Mamlaka nchini Kenya, zimesema kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na mvua na mafuriko yanayoendelea kushuhudiwa nchini humo, imeongezeka na kufikia watu 228, wataalamu wakionya kuwa hatari ya maafa zaidi bado iko.

Athari za mvua kubwa iliosababisha mafuriko katika mji Mai Mahiu, Kenya, on 29 April, 2024.
Athari za mvua kubwa iliosababisha mafuriko katika mji Mai Mahiu, Kenya, on 29 April, 2024. AFP - LUIS TATO
Matangazo ya kibiashara

Wakati huu Kenya na jirani yake Tanzania, wakinusurika na madhara makubwa ya kimbunga Hidaya ambacho kilipungua kasi yake siku ya Jumamosi, Serikali ya Nairobi imesema mvua kubwa bado zitashuhudiwa na kwamba kuna hatari ya mafuriko zaidi.

Hapo jana eneo la magharibi mwa Kenya hasa kwenye mji wa Kisumu, raia walijipata matatani baada ya barabara kuu ya mji huo na Nairobi kulazimika kufungwa baada ya mto Nyando kupasuka kiongo zake na kuharibu miondombinu kadhaa kwenye mji wa Ahero.

Mwanamume akiongoza mifugo wake kwenye maji ya mafuriko huko Kisumu, Kenya Jumatano, Aprili 17, 2024. Mvua kubwa inayonyesha katika maeneo tofauti ya Kenya imesababisha vifo vya takriban watu 13 na wengine 15,000 kuwa wakimbizi, Umoja wa Mataifa ulisema, huku watabiri wa hali ya hewa wakionya mvua kubwa itaendelea hadi Juni. (Picha ya AP/Brian Ongoro)
Mwanamume akiongoza mifugo wake kwenye maji ya mafuriko huko Kisumu, Kenya Jumatano, Aprili 17, 2024. Mvua kubwa inayonyesha katika maeneo tofauti ya Kenya imesababisha vifo vya takriban watu 13 na wengine 15,000 kuwa wakimbizi, Umoja wa Mataifa ulisema, huku watabiri wa hali ya hewa wakionya mvua kubwa itaendelea hadi Juni. (Picha ya AP/Brian Ongoro) AP - Brian Ongoro

Majuma kadhaa ya mvua za msimu ambazo safari hii zimekuja kwa kiwango cha juu zikichangiwa na kipindi cha El Nino, zimesababisha sintofahamu kwenye ukanda mzima wa Afrika Mashariki, ambao umeathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Soma piaMafuriko nchini Kenya: Vitongoji duni vyabomolewa ili kulazimisha watu kuhama

Zaidi ya watu 400 wameripotiwa kufa na wengine mamia kupoteza makazi kwenye nchi za Kenya, Tanzani na Burundi, huku miundombinu mingi ikiwemo shule na barabaraza ikiharibiwa vibaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.