Pata taarifa kuu

Uingereza: Mahakama yaamuru dhidi ya kufukuzwa kwa wahamiaji kwenda Rwanda

Uingereza haitapeleka waomba hifadhi wake nchini Rwanda. Ilikuwa sera kuu ya Boris Johnson na mrithi wake, Rishi Sunak: kutoa mfumo wake wa hifadhi kwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki, hatua ambayo ilishutumiwa sana na upinzani na wanaharakati. Mahakam imefutilia mbali mradi wa serikali. Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak ametangaza kuwa serikali yake inakusudia kupinga uamuzi wa Mahakama ya Rufaa mbele ya Mahakama ya Juu.

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakiwa 10 Downing Street London, Uingereza, Alhamisi, Mei 4, 2023.
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakiwa 10 Downing Street London, Uingereza, Alhamisi, Mei 4, 2023. © Stefan Rousseau / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Rwanda si nchi ya tatu salama: ni hitimisho la Mahakama ya Rufaa, ambayo kwa hiyo inafanya mradi wa serikali kuwa haramu, anaripoti mwandishi wetu wa London, Émeline Vin. Majaji watatu wanasema wanaotafuta hifadhi hawatakuwa salama kabisa nchini Rwanda: katika hukumu ya kurasa 160, mahakama inaona hatari ya wahamiaji kurejeshwa katika nchi yao ya asili wakati wakisubiri ombi lao kutathminiwa.

Hata hivyo, mahakama inaacha mlango wazi kwa utekelezaji wa sera hiyo, "ikiwa Kigali itarekebisha dosari katika mchakato wake wa kupata hifadhi". "Ninaheshimu mahakama, lakini kimsingi sikubaliani na matokeo yake," kiongozi huyo wa Conservative amesema katika taarifa yake. “Rwanda ni nchi salama. Sasa tutaomba kibali cha kukata rufaa dhidi ya uamuzi huu kwa Mahakama ya Juu,” ameongeza Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak.

Nakala yachukuliwa kuwa sio ya kibinadamu

Mnamo mwezi Desemba, Mahakama Kuu hata hivyo iliidhinisha nakala hiyo, kabla ya Mahakama ya Rufaa kuiidhinisha. Watetezi wa haki za wahamiaji walishutumu ripoti ya haki za binadamu nchini Rwanda. Upinzani, ambao ulishindwa kuzuia mradi huo Bungeni, uliona kuwa haufai, na sio wa kibinadamu na zaidi ya yote ni ghali sana: mwanzoni mwa juma, Wizara ya Mambo ya Ndani ilikadiria euro 200,000 kama gharama ya kuhamisha kila mwomba hifadhi, kutoka Uingereza.

Serikali imefanya kupunguka kwa idadi ya wahamiaji haramu hasa moja ya ahadi zake za kampeni. Ushirikiano na Rwanda ulikuwa kama kizuizi.

Serikali ya Rwanda imetangaza kwamba bado inajitolea kwa makubaliano na London kutoa uhamishaji wa wahamiaji haramu kutoka Uingereza kwenda Rwanda, ingawa mahakama ya Uingereza imetangaza kuwa ni "kinyume cha sheria". "Wakati uamuzi huu hatimaye uko kwa mahakama za Uingereza, tunapinga ukweli kwamba Rwanda haichukuliwi kuwa nchi salama kwa wakimbizi na wanaotafuta hifadhi," msemaji wa serikali ya Rwanda, Yolande Makolo, ameliambia shirika la habari la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.