Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza nchini Rwanda kuimarisha mpango wa uhamiaji

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza Suella Braverman yuko katika ziara rasmi mjini Kigali tangu Jumamosi hii na Jumapili Machi 19. Takriban mwaka mmoja baada ya kusainiwa kwa mkataba wa wakimbizi wa karibu Euro milioni 160 kati ya Rwanda na Uingereza, lengo ni kurejesha ahadi ya London kwa ushirikiano huu. London inatarajia kutuma nchini Rwanda idadi fulani ya waomba hifadhi waliowasili kinyume cha sheria katika ardhi ya Uingereza.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza Suella Braverman akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu Kigali, Rwanda, Jumamosi, Machi 18, 2023.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza Suella Braverman akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu Kigali, Rwanda, Jumamosi, Machi 18, 2023. AP
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Kigali, Lucie Mouillaud

Hii ni ziara ya kwanza rasmi mjini Kigali kwa mjumbe wa serikali ya Uingereza tangu kuchaguliwa Rishi Sunak kutoka chama cha kihafidhina mwezi Oktoba mwaka jana. Fursa kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Vincent Biruta, kusisitiza ahadi yake kwa Uingereza.

“Tumemaliza mkutano ambapo tulijadili ushirikiano wetu kuhusu uhamiaji na maendeleo ya kiuchumi. Ushirikiano huu wa kibunifu unawakilisha maendeleo muhimu katika juhudi zetu za kushughulikia uhamiaji haramu. Na tunafurahi kufanya kazi bega kwa bega na Uingereza juu ya hili. »

Mjini Kigali, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza alitembelea makaazi mapya, yaliyokusudiwa kuwahudumia wakimbizi waliotumwa Rwanda na Uingereza. Makubaliano kati ya nchi hizo mbili, yaliyotangazwa kisheria na Mahakama Kuu ya Uingereza mwezi Desemba, bado yanapingwa mahakamani na kundi la waomba hifadhi. Lakini kulingana na Suella Braverman, Uingereza inatarajia kutekeleza ushirikiano wake na Rwanda haraka iwezekanavyo.

“Leo tumetia saini kwa mara nyinge ya makubaliano yetu ambayo yanaongeza hatua za kusaidia watu ambao watahamishiwa Rwanda. Kuna mgogoro wa uhamiaji duniani, na ninaamini kwa dhati kwamba ushirikiano huu kati ya washirika wawili na marafiki wawili utaongoza njia. "

Kesi hii ya wahamiaji imepangwa kusikilizwa katikati ya mwezi wa Aprili kuchunguza utaratibu uliozinduliwa katika Mahakama ya Rufaa dhidi ya mkataba huu, ambao bado unashutumiwa na mashirika mengi ya haki za binadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.