Pata taarifa kuu

Uganda kurejesha mabaki ya mashujaa wa kikristo waliouawa

Uganda itarejesha nyumbani mabaki ya "mashujaa wawili wa Uganda" waliouawa zaidi ya karne moja iliyopita kwa kukataa kuukana Ukristo, afisa wa Kanisa alitangaza siku ya Jumapili.

Papa Francis atembelea Madhabahu ya Mashahidi wa Uganda huko Namugongo, tarehe 28 Novemba, 2015.
Papa Francis atembelea Madhabahu ya Mashahidi wa Uganda huko Namugongo, tarehe 28 Novemba, 2015. D.Lubowa.jpg
Matangazo ya kibiashara

Wakatoliki 22 na Waanglikana 23, wengi wao wakiwa vijana, waliuawa katika miaka ya 1885 na 1886 kwa amri ya mfalme wa Buganda, eneo ambalo sasa ni sehemu ya Uganda, kwa sababu hawakuamini ushawishi unaokua wa Ukristo. Wanaume hawa wote walikufa kifo cha kutisha: wengi walichomwa wakiwa hai, wengine waliuawa kwa mikuki au visu.

The White Fathers, jumuiya ya Kikatoliki ya Kirumi ambayo pia inajulikana kama Wamisionari wa Afrika, ilipeleka mabaki ya mashujaa wawili wa imani huko Roma ambako baadaye walitangazwa kuwa watakatifu Oktoba 1964, na wengine walihifadhiwa nchini Uganda.

"Tarehe ya kurejeshwa kwa mabaki na masalia bado haijatangazwa lakini kuna uwezekano mkubwa itakuwa mwezi Septemba mwaka huu," Padre Richard Nyombi wa Jimbo Kuu la Kampala, pia mwanachama wa White Fathers, ameliambia shirika la habari la AFP.

Mifupa itakayorejeshwa Uganda ni ya Charles Lwanga na Matiya Mulumba, Padri Nyombi amesema na kuongeza kuwa itaonyeshwa katika Chuo Kikuu cha Mashujaa wa  Uganda pamoja na vitu vikiwemo mnyororo uliotumika wakati wa kunyongwa kwao na msalaba uliotengenezwa kwa mbao za mvule.

Kurudi kwao ni sehemu ya ukumbusho wa mwaka wa 60 wa tarehe ambayo Wakatoliki walifanywa watakatifu na Papa Paulo VI. Hekalu lilianzishwa katika eneo walikouawa huko Namugongo, kitongoji cha Kampala, mji mkuu wa Uganda.

Namugongo ni sehemu muhimu ya hija ya Kikristo ambapo waumini wengi kutoka kote barani Afrika na kwingineko duniani wanaenda Juni 3, kwa kurejelea tarehe ambayo mauaji mengi yalifanywa mnamo mwaka 1886. 

Mabaki ya watu kadhaa hayajapatikana kwa sababu ya kuliwa na wanyama pori baada ya kuuawa, Padri Nyombi amebainisha. Kurejeshwa kwa mifupa hiyo kutoka Roma kutakuwa kwa wakati muafaka, ameongeza, na kuwapa waumini fursa ya kutafakari juu ya maadili ya wahanga wakati huu ambapo “Uganda inakabiliwa na changamoto kadhaa, matatizo ya kiuchumi, kuzorota kwa maadili na rushwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.