Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Charles III aanza ziara ya kiserikali nchini Kenya

Mfalme Charles III anaanza ziara ya kiserikali nchini Kenya leo Jumanne, ambapo atakabiliwa na matakwa mengi ya kuomba radhi kwa ukoloni wa zamani wa Uingereza katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Wanafamilia wa wapigania uhuru, Mau Mau, wakati wa maandamano, Jumatatu, Oktoba 30, 2023, kupinga ziara ya Charles III wa Uingereza na Malkia Camilla, nchini Kenya.
Wanafamilia wa wapigania uhuru, Mau Mau, wakati wa maandamano, Jumatatu, Oktoba 30, 2023, kupinga ziara ya Charles III wa Uingereza na Malkia Camilla, nchini Kenya. REUTERS - MONICAH MWANGI
Matangazo ya kibiashara

Ziara hiyo ya siku nne, ambayo inakuja kabla ya Kenya kuadhimisha miaka 60 ya uhuru mwezi Desemba, ni ya kwanza kwake kama mfalme katika nchi ya Jumuiya ya Madola. "Ziara hiyo inatoa ishara kwa ushirikiano thabiti na wenye kudumu kati ya Uingereza na Kenya," ubalozi wa Uingereza umesema katika taarifa.

Lakini ziara ya Mfalme Charles III, 74, na Malkia Camilla, 76, pia itafanya iwezekane kujadili "mambo mabaya ya historia ya pamoja ya Uingereza na Kenya" katika miaka iliyotangulia uhuru, Kasri la  Buckingham Palace limebaini.

Kati ya mwaka 1952 na 1960, zaidi ya watu 10,000 waliuawa nchini Kenya kufuatia uasi wa Mau Mau dhidi ya mamlaka ya kikoloni, mojawapo ya ukandamizaji wa umwagaji damu zaidi wa ufalme wa Uingereza.

Baada ya miaka mingi ya kesi, London ilikubali mwaka 2013 kuwafidia zaidi ya Wakenya 5,000, lakini baadhi wanasubiri mfalme aombe msamaha rasmi kwa hatua za awali za Uingereza.

- "Msamaha usio na shaka" -

"Tunamwomba Mfalme, kwa niaba ya Serikali ya Uingereza, kuomba msamaha wa umma bila masharti na bila shaka (...) kwa unyanyasaji wa kikatili na wa kinyama kwa raia wa Kenya katika kipindi chote cha ukoloni", kati ya mwaka 1895 na 1963, hivi karibuni KHRC, kundi huru la haki za binadamu lilisema.

KHRC pia ilidai fidia "kwa ukatili wote uliofanywa dhidi ya makundi mbalimbali nchini", ikitaja, pamoja na ukandamizaji wa Mau Mau, unyakuzi wa ardhi.

Baada ya kuwasili Kenya Jumatatu jioni, Charles na Camilla watapokelewa Jumanne katika mji mkuu Nairobi na Rais William Ruto, ambaye alikaribisha, katika ziara hii ya mfalme na mkewe, "fursa muhimu ya kuimarisha ushirikiano" katika nyanja tofauti.

Kwenye aajenda ya ziara yake kwa siku hizi mbili: Mfalme Charles atakutana na wajasiriamali, vijana, karamu ya serikali, kutembelea jumba jipya la kumbukumbu lililowekwa kwa historia ya Kenya na kuweka shada la maua kwenye kaburi la askari asiyejulikana katika bustani za Uhuru.

Mfalme na mkewe watazuru jiji la bandari la Mombasa (kusini), ambapo Charles, anayehusika na masuala ya mazingira, atatembelea hifadhi ya asili na kukutana na wawakilishi wa kidini.

Baada ya ziara za serikali nchini Ujerumani na kisha Ufaransa, kuashiria nia ya London ya kukaribiana na washirika wake wa Ulaya, Charles aligeukia Jumuiya ya Madola.

Salio hili la himaya ya Uingereza ambayo inazileta pamoja nchi 56, nyingi zikiwa makoloni ya zamani ya Uingereza, inadhoofishwa na ukosoaji mkubwa unaoendelea wa ukoloni wa Uingereza.

Ziara zingine za familia ya kifalme kwa makoloni ya zamani zimezua taharuki. Katika visiwa vya Caribbean mwaka jana, Prince William na Kate walitakiwa kuomba msamaha kwa utumwa wa Uingereza wa zamani.

Kenya inashikilia nafasi maalum katika historia ya familia ya kifalme ya Uingereza. Ni katika nchi hii ambapo mamake Charles, Elizabeth II, alifahamu kuhusu kifo cha baba yake George VI mwaka wa 1952 na akawa malkia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.