Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Charles III nchini Kenya kwa ziara yake ya kwanza katika nchi ya Jumuiya ya Madola

Mfalme wa Uingereza Charles III anaanza ziara yake ya kwanza nchini Kenya siku ya Jumanne, akiwa na mwelekeo mkubwa wa hisia, kama mfalme katika nchi ya Jumuiya ya Madola, wakati ambapo taasisi hii inaonekana kudhoofika na wakati wito unaongezeka kwa Uingereza kukabiliana na ukoloni wake wa zamani.

Mfalme Charles III na Malkia Camilla watapokelewa na rais William Ruto katika mji mkuu wa Nairobi siku ya Jumanne.
Mfalme Charles III na Malkia Camilla watapokelewa na rais William Ruto katika mji mkuu wa Nairobi siku ya Jumanne. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kenya inahusishwa hasa na historia ya familia ya kifalme: ni hapo mwaka wa 1952, Elizabeth II alipopata habari kuhusu kifo cha babake, Mfalme George VI, na kumfanya kuwa Malkia mpya wa Uingereza. Ziara ya Charles III na Malkia Camilla itafanyika wiki chache kabla ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki kuadhimisha miaka 60 ya uhuru wake, uliyotangazwa Desemba 12, 1963.

Mfalme Charles III na Malkia Camilla watapokelewa na rais William Ruto katika mji mkuu wa Nairobi siku ya Jumanne. Kwa siku mbili, watakutana kwa mazungumzo na wajasiriamali na vijana, watashiriki karamu ya serikali, watembelee jumba jipya la makumbusho linalohusu historia ya Kenya na kuweka shada la maua kwenye kaburi la askari asiyejulikana katika bustani ya Uhuru.

Kisha, Charles na Camilla wataenda Mombasa, kusini mwa nchi, ambako mfalme, anayehusika na masuala ya mazingira, atatembelea hifadhi ya asili na kukutana na wawakilishi wa dini mbalimbali.

Baada ya kuonyesha nia ya London ya kukaribiana na washirika wake wa Ulaya na ziara zake za serikali nchini Ujerumani na Ufaransa, Charles III, kwenye kiti cha enzi kwa zaidi ya mwaka mmoja, anazindua "dhamira yake ya kuokoa Jumuiya ya Madola" nchini Kenya. ", Gazeti la kila siku la Daily Mail limeripoti.

Taasisi hii inaleta pamoja nchi 56, nyingi zikiwa makoloni ya zamani ya Uingereza, na kati yao, falme 15 (ikiwa ni pamoja na Uingereza, Australia, Bahamas, Canada na New Zealand) ambazo bado zina mfalme kama mkuu wa nchi. Lakini katika baadhi yao, wazo la kuwa Jamhuri, kama Barbados mnamo 2021, linakua, kama huko Jamaica na Belize.

Msamaha unatarajiwa

Elizabeth II, ambaye alifanya ziara ya kiserikali nchini Kenya mwaka wa 1983, "alihusishwa sana na Jumuiya ya Madola na nadhani serikali ya Uingereza ilitarajia mfalme kuwa na mtazamo sawa na kujaribu kuukuza na kuhifadhi umoja wake", anasema Poppy Cullen, mwanahistoria katika Chuo Kikuu cha Cambridge.

Kwa mujibu wa London, ziara hii nchini Kenya ni fursa ya "kuonyesha jamhuri huru ndani ya Jumuiya ya Madola, ambayo bado inanufaika na uhusiano wake na Uingereza", na kuiwasilisha labda kama "kielelezo kinachowezekana kwa nchi "nyingine", ameongeza Poppy Cullen akiohojiwa na shirika la habari la AFP. "Ziara hii inaonyesha kina cha uhusiano wetu na ushirikiano wetu na manufaa ya pamoja", amesema Rais Ruto kwenye X (zamani ikiitwa Twitter) kabla ya kuwasili kwa Charles III.

Historia kati ya nchi hizo mbili haikosi nyakati za giza kama vile ukandamizaji wa uasi wa Mau Mau, ambao ulisababisha vifo vya zaidi ya watu 10,000 kati ya mwaka 1952 na 1960, hasa kutoka kwa jamii ya Wakikuyu, mojawapo ya ukandamizaji mkali zaidi wa utawala wa Uingereza

Baada ya miaka mingi ya kesi, London ilikubali mwaka wa 2013 kuwafidia Wakenya zaidi ya 5,000, lakini baadhi wanasubiri mfalme atoe msamaha rasmi kwa hatua za awali za Uingereza. Hata leo, kuwepo kwa wanajeshi wa Uingereza kunazua mvutano na Bunge la Kenya hivi majuzi lilianzisha uchunguzi unaolenga jeshi la Uingereza.

Ziara hii itakuwa fursa ya kujadili "mambo chungu nzima" ya historia kati ya nchi hizo mbili na Charles III "atachukua muda (...) kuongeza uelewa wake wa dhulma zilizowasibu raia wa Kenya katika kipindi hiki" , limebaini Kasri la Buckingham Palace kabla ya ziara yake.

Wakati familia ya kifalme inashutumiwa kwa ubaguzi wa rangi na binti-mkwe wa Charles, Meghan Markle, mfalme tayari ameonyesha nia ya kutuliza uhasama huo tangu kutawazwa kwake kwa kiti cha ufalme. Ziara zingine za familia ya kifalme kwa makoloni ya zamani zimezua taharuki. Katika visiwa vya Caribbean mwaka jana, Prince William na Kate waliitwa kuomba msamaha kwa utumwa wa Uingereza wa zamani.

Maoni haya "yalitoa matarajio mengi juu ya kile ambacho inaweza kumaanisha. Je, ataomba msamaha kweli?", Amesema Poppy Cullen. "Maneno yake yatasikilizwa kwa makini sana", na pengine nje ya Kenya, anabainisha mwanahistoria huyo: "Makoloni yote ya zamani yatafuatilia (ziara hii). Ikiwa mfalme ataomba msamaha au kuonyesha majuto kwa kipindi cha ukoloni nchini Kenya ( ...) hii itakuwa aina ya mfano mzuri."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.