Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Charles III na Camilla kuzuru Kenya mwishoni mwa mwezi

Charles III na mkewe Camilla watafanya ziara ya kiserikali nchini Kenya kuanzia Oktoba 31 hadi Novemba 3, ikiwa ni ziara ya kwanza ya mfalme huyo katika nchi ya Jumuiya ya Madola tangu kutawazwa kwake, Kasri la Buckingham limetangaza Jumatano.

Mfalme Charles III na Malkia Camilla huko Notre-Dame de Paris, Septemba 21, 2023.
Mfalme Charles III na Malkia Camilla huko Notre-Dame de Paris, Septemba 21, 2023. © Christophe Petit Tesson / AP
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii, kwa mwaliko wa rais wa Kenya William Ruto, itakuwa fursa ya "kusherehekea uhusiano mzuri kati ya nchi hizo mbili na ushirikiano thabiti na ulio imara ambao unaendelea kati ya nchi hizi mbili," Kasri la Buckingham limesema katika taarifa. Ziara hii Itafanyika takriban mwezi mmoja na nusu baada ya ziara ya Charles III na mkewe nchini Ufaransa na huku Kenya ikijiandaa kusherehekea maadhimiosho ya miaka 60 ya uhuru wake, uliotangazwa mnamo Desemba 12, 1963.

Ziara ya kwanza ya Charles III kama mfalme itafanyika "katika nchi ambayo utawala wa Malkia Elizabeth II ulianza", mnamo mwezi wa Februari 1952, Kasri la Buckingham imebainisha. Wakati huo binti mfalme, alikuwa nchini Kenya kama sehemu ya ziara ya Jumuiya ya Madola wakati babake Mfalme George VI alipofariki.

Charles na Camilla watatembelea mji mkuu Nairobi na mikoa ya Mombasa (kusini). Mpango wao "utaakisi jinsi Kenya na Uingereza zinavyofanya kazi pamoja, ikiwa ni pamoja na kuimarisha ustawi wa pande zote, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, kukuza fursa za vijana na ajira, kuendeleza maendeleo endelevu na kuunda kanda imara na salama," Kasri la Buckingham limeongeza.

Mfalme na Malkia watakutana na rais William Ruto na mkewe, wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, viongozi wa kidini na vijana.

Ziara hiyo pia itakuwa fursa ya kujadili "mambo yanayoudhi ya historia ya pamoja ya Uingereza na Kenya" katika miaka ya kabla ya uhuru, Kasri la Buckingham limesema. Kati ya miaka ya 1952 na 1960, zaidi ya watu 10,000 waliuawa nchini Kenya kufuatia uasi wa Mau Mau dhidi ya mamlaka ya kikoloni, mojawapo ya ukandamizaji wa umwagaji damu zaidi wa Milki ya Uingereza.

Charles III na Camilla watatembelea eneo ambapo uhuru ulitangazwa. Hii ni ziara rasmi ya nne ya Charles nchini. Ni nchini Kenya pia ambapo Prince William, mrithi wa kiti cha ufalme, alimtaka Kate Middleton awe mke wake mtarajiwa mnamo 2010.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.