Pata taarifa kuu

Kenya: Wamasai wanadai fidia kutoka kwa Charles III kwa uharibifu wa ufalme wa Uingereza

Wawakilishi wa jamii za Wamasai nchini Kenya na Tanzania walituma ombi kwa Ufalme wa Uingereza Jumapili Oktoba 29. Mfalme Charles III anatarajiwa kuwasili Nairobi siku ya Jumatatu kwa ziara ya siku nne. Kasri ya Buckingham ilitangaza kwamba mfalme huyo atajadili "mambo yenye uchungu zaidi" ya historia ya Uingereza nchini Kenya. Miongoni mwa mambo hayo, kulingana na jamii za Wamasai, ni kupokonywa ardhi zao.

Wawakilishi wa jamii za Wamasai wa Kenya na Tanzania wanamwomba Mfalme Charles III kusaidia kurejeshewa ardhi zao walizonyang'anywa ufame wa Uingereza mwanzoni mwa karne ya 20.
Wawakilishi wa jamii za Wamasai wa Kenya na Tanzania wanamwomba Mfalme Charles III kusaidia kurejeshewa ardhi zao walizonyang'anywa ufame wa Uingereza mwanzoni mwa karne ya 20. © RFI / Gaëlle Laleix
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Nairobi, Gaëlle Laleix

Mnamo 1904 na 1911, wakati Kenya ilikuwa chini ya enzi za ukoloni, mamlaka ya Uingereza iliwashinikiza wazee wa Kimasai kutia saini mikataba miwili, ambayo waliwapa walowezi mashamba yao. Wamasai walihamishwa kwenda katika hifadhi.

Leo, Daniel, mmoja wa machifu wa Wamasai wa Narok, kusini-magharibi mwa Nairobi, anadai haki: “Makubaliano haya yalianza kutekelezwa bila uwakilishi halisi wa jamii ya Wamasai na bila makubaliano yao. Hii imesababisha kunyang'anywa kwa sehemu kubwa ya ardhi ya mababu zetu, na kuhamishwa kwa watu wegi na changamoto za kijamii na kiuchumi kuzikumba jamii zetu. Wizi huu wa ardhi yetu umevuruga mfumo wetu wa maisha, umesambaratisha urithi wetu wa kitamaduni na kudhoofisha maisha yetu na ya vizazi vijavyo. "

Ili kurekebisha historia, Wamasai kwa hiyo waliwasilisha idadi fulani ya maombi kwa Mfalme Charles wa Tatu. Richard Legyagu, mshiriki wa baraza la wazee la Samburu, katikati mwa nchi, anaeleza: “Hatukuwahi kutia sahihi hati za uhuru katika Lancaster House, na tungependa fursa ya kufanya hivyo. Wamasai wa Tanzania wanamwomba mfalme atumie ushawishi wake kwa Tanzania ili kukomesha unyang'anyi wa mashamba yao ya Ngorongoro. Tunamuomba Mfalme atambue dhuluma za kihistoria walizofanyiwa Wamasai. Hatimaye, tunapendekeza mpango wa kina wa kurejesha ardhi na fidia. »

Wakati wa ziara yake, Mfalme Charles III hatakwenda katika maeneo wanakoishi Masai. Atakaa kwa siku mbili Nairobi, kisha atasafiri kwa ndege hadi Mombasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.