Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Mauaji ya Kimbari nchini Rwanda: Kesi ya Kabuga yasitishwa kwa sababu za kiafya

Majaji wa Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa walisitisha kesi ya Félicien Kabuga, anayedaiwa kuwa mfadhili wa mauaji ya halaiki nchini Rwanda mwaka 1994, muda wa kuamua kama afya yake inamruhusu kuendelea kusalia kizimbani.

Félicien Kabuga wakati wa akisikilizwa katikakesi yake mbele ya ICC, mjini Hague, Septemba 29, 2022.
Félicien Kabuga wakati wa akisikilizwa katikakesi yake mbele ya ICC, mjini Hague, Septemba 29, 2022. AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

Mahakama yenye makao yake mjini Hague imesema kuwa imepokea ripoti huru ya matibabu kuhusu hali ya afya ya mshukiwa kuhukumiwa, na itasikiliza kesi hiyo baadaye mwezi huu.

Mwanzoni mwa kesi ya Bw Kabuga mnamo mwezi Septemba 2022, waendesha mashtaka walimshtumu kwa jukumu kubwa katika mauaji ya halaiki, ikiwa ni pamoja na kutoa mapanga kwa wingi na kusimamia kituo cha Televisheni cha RTLM "Radio télévision libre des Mille collines", ambacho kilikuwa kikitoa wito wa mauaji dhidi ya Watutsi. .

Mfanyabiashara huyo, mwenye umri wa karibu miaka 88, alikataa kufika mahakamani au kusikilizwa kwa njia ya mtandao mwanzoni mwa kesi yake na baadaye alishiriki kwa njia ya video, kwenye kiti cha magurudumu, kutoka eneo anakozuiliwa huko Hague.

"Inafaa kesi hii isitishwe kwa vikao vya ushahidi kusubiri utatuzi wa suala la kufaa kwa Bw. Kabuga kujibu mashtaka," Jaji Kiongozi Iain Bonomy alisema katika agizo la mahakama.

Wataalamu watatu wa kitiba walioandika ripoti hiyo wametakiwa kutoa ushahidi mbele ya majaji, kuanzia wiki ijayo hadi Machi 29, ili kuongoza uamuzi wa mahakama "katika siku zijazo za kesi hii", aliongeza Bw. Bonomy.

Upande wa mashtaka na utetezi utashughulikia suala hilo mahakamani, alisema. Alipokamatwa mwaka wa 2020 karibu na mji wa Paris baada ya kuwa mafichoni kwa miaka 25, Bw. Kabuga anadaiwa kushiriki katika uundaji wa wanamgambo wa Kihutu wa Interahamwe, tawi lenye silaha la utawala wa wa Kihutu waliohusika katika mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani.

Félicien Kabuga alikanusha mashtaka kwamba alihusika, katika kituo cha redio cha Wahutu wenye itikadi kali, akihimiza kuuawa kwa 'mende' wa Kitutsi wakati wa mauaji ya 1994 ambapo watu 800,000 waliuawa. Pia alikana kutoa mapanga au kuunga mkono wanamgambo wa Kihutu Interahamwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.