Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Felicien Kabuga kuanza kusikilizwa mbele ya mahakama ya ICC

Kesi dhidi ya Felicien Kabuga, raia wa Rwanda, itaanza katika mahakama ya kimataifa ya mjini Hague, nchini Uholanzi, anakotuhumiwa kufadhili mauaji ya kimbari ya mwaka 1994. 

Felicien Kabuga alisaidia kuundwa kwa iliyokuwa redio mashuhuri Radio-Television Libre des Mille Collines, ambayo ilitumika kuchochea watu kuwaua Watutsi, ambapo alikuwa rais wake.
Felicien Kabuga alisaidia kuundwa kwa iliyokuwa redio mashuhuri Radio-Television Libre des Mille Collines, ambayo ilitumika kuchochea watu kuwaua Watutsi, ambapo alikuwa rais wake. AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, fedha zake na uhusiano aliokuwa nao na watu mbalimbali duniani, zilimsaidia kukwepa mkono wa sheria kwa zaidi ya miaka 20, ambapo aliishi Uswisi, DRC na Kenya kwa nyakati tofauti. 

Mwaka 1993, mmoja ya watoto wake wakike, aliolewa na mtoto mkubwa wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Juvenal Habyarimana, ambaye kuuawa kwake kulisababisha machafuko ya mwaka 1994. 

Mtoto Wake mwingine aliolewa na Augustine Ngirabatware, waziri wa mipango aliyehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kuhusika kwenye mauaji hayo. 

Aidha Kabuga, alisaidia kuundwa kwa iliyokuwa redio mashuhuri Radio-Television Libre des Mille Collines, ambayo ilitumika kuchochea watu kuwaua Watutsi, ambapo alikuwa rais wake. 

Kabuga pia anatuhumiwa kusimamia mauaji ya Interahamwe kwenye mji wa Gisenyi, kaskazini magharibi mwa Rwanda pamoja na wilaya ya Kimironko. 

Mawakili wa Kabuga, mara kadhaa wamejaribu bila mafanikio kutaka mteja wao asisimame kizimbani kwa kisingizio cha kuwa na umri mkubwa wa miaka 80. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.