Pata taarifa kuu
ICC-HAKI

Félicien Kabuga kuhukumiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Hague

Félicien Kabuga, mfanyibiashara wa Rwanda aliyekamatwa nchini Ufaransa mwaka 2020 akihusishwa na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 amepelekwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Hague badala ya Mahakama maalum kuhusu mauaji hayo yaliyopo, Arusha ili kufunguliwa mashtaka kwa sababu ya kudhoofika kwa hali yake ya kiafya.

Wakili wa Felicien Kabuga, Emmanuel Altit, amesema kwamba watawasilisha ombi la mteja wao kupelekwa katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC mjini The Hague baada ya mahakama kuu ya Ufaransa kuunga mkono uamuzi wa mshukiwa huyo kushtakiwa nchini Tanzania.
Wakili wa Felicien Kabuga, Emmanuel Altit, amesema kwamba watawasilisha ombi la mteja wao kupelekwa katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC mjini The Hague baada ya mahakama kuu ya Ufaransa kuunga mkono uamuzi wa mshukiwa huyo kushtakiwa nchini Tanzania. Mecanisme pour les Tribunaux penaux internationaux/Nations Unies/AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Kabuga mwenye umri wa miaka 84, amekuwa mafichoni kwa zaidi ya miongo miwili na ni mtu anaesakwa zaidi ulimwenguni. Anatuhumiwa kwa kuchochea mauaji ya Watutsi 800,000 pamoja na Wahutu wenye msimamo wa wastani.

Miaka hiyo Kabuga alikuwa akizingatiwa kama mtu tajiri zaidi Rwanda. Na anadaiwa alitumia utajiri wake kuanzisha vyombo vya habari vilivyokuwa vikisambaza taarifa za chuki zilizokuwa zikiwachochea Wahutu kuwauwa wenzao wa kabila la Tutsi kwa kutumia maneno ya propaganda na kuwaita mende ili kuwatoa utu wao, iwe rahisi kuwaua.

Alikamatwa karibu na mji wa Paris mnamo Mei 16 na anakabiliwa na mashtaka ya mwaka 1997 ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Rwanda (ICTR) iliyofungwa sasa. Kabuga alihamishwa kutoka Ufaransa kwenda mjini The Hague mnamo mwezi Oktoba.

Kufuatia kukamatwa kwake, mawakili wake walitaka kesi yake isikilizwe nchini Ufaransa, lakini mahakama ya juu nchini humo imeamrisha kesi hiyo ihamishiwe kwenye mahakama ya Umoja wa Mataifa.

'Hatutaki Kabuga ashtakiwe Tanzania'

Wakili wa Félicien Kabuga, Emmanuel Altit, amesema kwamba watawasilisha ombi la mteja wao kupelekwa katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC mjini The Hague baada ya mahakama kuu ya Ufaransa kuunga mkono uamuzi wa mshukiwa huyo kushtakiwa nchini Tanzania.

Bwana Kabuga amedaiwa kufadhili makundi ya wapiganaji akiwa mwenyekiti wa hazina ya kitaifa ya ulinzi .

Félicien Kabuga alikamatwa mjini Paris mnamo mwezi Mei baada ya kutoroka kwa miaka 26 ambapo maafisa wa polisi wanasema alitumia majina 28 tofauti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.