Pata taarifa kuu

Omicron : Visa vya maambukizi vyaripotiwa Rwanda na Kenya

Rwanda na Kenya, yamekuwa mataifa ya hivi punde ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, baada ya Uganda, kuripoti visa vya kirusi kipya cha Covid-19 cha Omicron kinachosambaa kwa kasi duniani.

Akizungumza wiki hii katika kongamano la afya kuhusu bara la Afrika, Kagame ametaka ushirikiano wa karibu kushinda kirusi cha Omicron.
Akizungumza wiki hii katika kongamano la afya kuhusu bara la Afrika, Kagame ametaka ushirikiano wa karibu kushinda kirusi cha Omicron. © Internet
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya afya nchini Rwanda imentangaza visa sita vya kirusi cha Omicron ambavyo vimebainika kutoka kwa abiria waliowasili nchini humo.

Kufuatia hatua hiyo, Baraza la mawaziri baada ya kukutana chini ya uongozi wa rais Paul Kagame, limepiga marufuku watu kukutana katika klabu za usiku, kuanzia siku ya Alhamisi, na wageni wanaowasili nchini humo watawekwa karatini kwa siku tatu badala ya saa 24 huku masharti ya watu kutotembea nje yakiendelea kuwepo mpaka saa 10 Alfajiri.

 Akizungumza wiki hii katika kongamano la afya kuhusu bara la Afrika, Kagame ametaka ushirikiano wa karibu kushinda kirusi cha Omicron.

Nchini Kenya, Waziri wa afya Mutahi Kagwe ametangaza kuwa visa vitatu vya kirusi hicho, pia vimebainika kutoka kwa abiria, mmoja raia wa Afrika Kusini na Wakenya wawili na wamewekwa karantini.

Mashaka yaliyopo kuhusu kuwepo kwa kirusi hiki cha Omicron ,ni ushahidi kuwa vita dhidi ya janga hili bado inaendelea, lazima tuendelee kuwa makini na kushirikiana haraka sana, kama bara la Afrika na washirika wetu duniani.

Wizara ya afya nchini Kenya imeendelea kutoa wito kwa watu nchini humo kuendelea kupokea chanjo, wakati huu Mahakama ikisimamisha mpango wa serikali kuwanyima huduma za serikali, watu ambao hawataonesha vyeti vya kupokea chanjo kuanzia Desemba 21.

Kirusi cha Omicron kiliripitiwa mara ya kwanza na shirika la Afya Duniani, WHO,  nchini Afrika Kusini Novemba 24.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.