Pata taarifa kuu

Covid nchini Uingereza: Vizuizi vipya vinaleta hofu kwa huduma ya afya ya umma

Hofu inaendelea kutanda Jumanne hii nchini Uingereza na tangazo la utekelezaji ujao wa pasi ya afya. Timu za NHS hazikuwa na wakati wa kujiandaa kwa wimbi kubwa la maombi ya vipimo na miadi ya kipimo cha tatu.

Nje ya kituo cha chanjo katika Hospitali ya Guy na St Thomas katikati mwa London, Desemba 13, 2021.
Nje ya kituo cha chanjo katika Hospitali ya Guy na St Thomas katikati mwa London, Desemba 13, 2021. AFP - TOLGA AKMEN
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati kunaripotiwa upungufu wa vipimo vya mtandaoni na katika maduka ya dawa. Kwa hivyo lazima upange foleni kwenye baridi, wakati mwingine zaidi ya saa sita katikati mwa London.

"Tunajaribu tusife kutokana na Covid na tuweze kufa kwa ugonjwa mwingine kama ugonjwa wa moyo na mishipa au saratani tunapokuwa wazee," mwanamume mmoja amesema. Kweli, ninajaribu kulichukulia kama mzaha. "

Serikali inatoa wito kwa kuvalia njuga suala la chanjo: watu 10,000 wamejitolea kusaidia kusimamia chanjo milioni 18 zilizoahidiwa kwa wale walio na umri wa zaidi ya miaka 18 kabla ya mwisho wa mwaka. Changamoto ya kweli kwa NHS.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.