Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Ripoti: Serikali ya Uingereza imefanya 'makosa makubwa' katika kudhibiti Covid-19

Vifo elfu kadhaa vimeweza kuepukwa. Kulingana na ripoti ya bunge inayokosoa usimamizi wa janga hilo, Uingereza imefanya "makosa makubwa". Hatua ya kwanza kukabiliana janga la Covid-19 ilianza imechelewa sana.

Wapita njia wakipita mbele ya bango lililoonya kwamba "idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona ni kubwa sana London", Desemba 19, 2020.
Wapita njia wakipita mbele ya bango lililoonya kwamba "idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona ni kubwa sana London", Desemba 19, 2020. © TOLGA AKMEN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Uingereza imerekodi vifo 138,000 kutokana na Covid-19,  ikiwa ni nchi ya kwanza kurekodi vifo vingi barani Ulaya. Serikali ya Uingereza haikuchukuwa hatua haraka, kulingana na ripoti iliyotolewa na kamati mbili za bunge baada ya vikao vilivyofanyika  kwa miezi kadhaa.

Mwanzoni, viongozi walitegemea kinga ya ya pamoja, na hivyo kuruhusu virusi kuenea kwa watu wengi, huku hospitali zikizidiwa kutokana an wingi wa waginjwa. Hospitali zililazimika kukataa kupokea wagonjwa, kwa sababu serikali ili ilichelewa kutangaza hatua za watu kutotembea. Uingereza ilichelewa kutangaza hatua hizo kwa wastani wa wiki mbili ikilinganishwa na majirani zake. Kauli mbiu wakati huo ilikuwa kulinda uchumi.

"Kulikuwa na fikra mbalimbali," amesema Jeremy Hunt, mbunge wa kutoka chama cha Conservative, waziri wa zamani wa afya na mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo. Hatimaye tulifikiri kwamba hii itakuwa njia pekee ya kukomesha virusi. Tungelipswa kuangalia mapema juu ya kile kilichotokea Korea Kusini na Taiwan: Walifanikiwa vzaidi kudhibiti virusi vya Corona. "

Maendeleo ya kisayansi sawa

Nchi ilifikiria kuwa nihoma ya mafua bila kujua kuwa huo ni ugonjwa mpya. Katika ngazi ya kisayansi, Uingereza iko mbele, imeandaa vipimo vya uchunguzi wa Covid kabla ya nchi yoyote. Lakini haikuweza kuzipeleka nchini kote haraka iwezekanavyo.

Habari njema katika ripoti hii, hata hivyo, ni kwamba sera ya chanjo ni moja wapo ya ufanisi zaidi ulimwenguni. Karibu 80% ya watu walio na umri wa miaka 12 na zaidi walipokea dozi mbili. Chanjo hiyo iligawanywa mapema mwezi Desemba mwaka uliopita.

Serikali haikuomba radhi. Walakini, waziri amesema: "Tumeazimia kujifunza kuhusiana na janga la Covid-19. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.