Pata taarifa kuu
UINGEREZA-COVID 19

Uingereza yatangaza kulegeza masharti ya kupambana na Covid 19

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametangaza kulegeza masharti ya kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya corona nchini humo.

Waziri Mkuu wa Uingereza  Boris Johnson
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson Jonathan Buckmaster POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Masharti  yanayolegezwa kuanzia Julai 19,  ni pamoja na kutovaa barakoa na kutokaa umbali wa mita moja, miongoni mwa masharti mengine kama ambavyo imekuwa ikishuhudiwa.

Hata hivyo, Johnson amewataka watu nchini humo kuendelea kuchukua tahadhari licha ya kulegezwa kwa masharti hayo, wakati utakapowadia.

Mafanikio ambayo tumeyapata kwa utoaji chanjo, yametuweka katika nafasi nzuri sana, ukilinganisha na mataifa mengine, katika vita vya kujilinda kama tulivyo sasa, lakini lazima tuendelee kuchukua tahadhari.

Hata hivyo, Johnnson amesema hatua ya mwisho ya kuthibitisha hatua hii, itaamuliwa tarehe 12 mwezi Julai.

Watu nchini humo wametakiwa kuendelea kuvaa barakoa katika maeneo yenye mikusanyiko kama hatua ya kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi hayo.

Watalaam wanasema, licha ya hatua hii ya serikali, maambukizi mapya yanatarajiwa kuongezeka na kufikia zaidi ya 50,000 kwa siku, mwezi Julai.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.