Pata taarifa kuu
UINGEREZA-AFYA

Mtaalam wa magonjwa: Mwisho wa Corona waweza kuwa karibu nchini Uingereza

Janga la COVID-19 linaweza kumalizika katika kipindi cha miezi michache ijayo nchini Uingereza, chanjo ikiwa imepunguza sana hatari ya kusababisha kifo au kudhoofika kupita kiasi kutoka na virusi hivyo, amesema mtaalam wa magonjwa ya kuambukia Neil Ferguson kutoka Chuo Kikuu cha Imperial College.

Wahudumu wa afya wakiwa katika kampeni ya chanjo kwa waendeshaji magari katika kituo cha magari cha "World of Adventures" huko Chessington, Uingereza, Machi 28, 2020..
Wahudumu wa afya wakiwa katika kampeni ya chanjo kwa waendeshaji magari katika kituo cha magari cha "World of Adventures" huko Chessington, Uingereza, Machi 28, 2020.. REUTERS/Peter Nicholls
Matangazo ya kibiashara

Amebainisha, hata hivyo, kwamba kushuka kwa idadi ya visa vya maambukizi ya kila siku  - ambayo ilikuwa juu zaidi kwa siku sita zilizopita - lazima izingatiwe kwa uangalifu.

Ujumbe umeungwa mkono na Waziri Mkuu Boris Johnson: "Ni dhahiri nimeona kwamba haali imebadilika kwa siku sita lakini ni muhimu sana, kutoharakia kujipa moyo na watu kuweza kujiachia," amesema Bw. Johnson.

"Lazima tuwe waangalifu na hii ndiyo nasaha ya serikali" ameaongeza.

Mlipuko wa sasa, ambao ulisababisha maambukizi mapya 54,674 katika masaa 24 Julai 17, umepungua, na visa vya maambukizi ya kila siku ya  24,950 yalirekodiwa Jumatatu wiki hii.

"Matokeo ya chanjo yamekuwa ni yenye ufanisi mkubwa katika kupunguza hatari ya kulazwa hospitalini au kifo na, kwa maoni yangu, nina hakika kwamba mwishoni mwa mwezi Septemba-au ma^pema mwezi Oktoba, janga kubwa litakuwa limetokomezwa," amesema mtaalam wa magonjwa ya kuambukia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.