Pata taarifa kuu
UINGEREZA-AFYA

Coronavirus: London yapanga kutoa chanjo ya lazima kwa wahudumu wa afya

Serikali ya Uingereza inafikiria kuifanya chanjo dhidi ya virusi vya Corona  kuwa ya lazima kwa wafanyakazi wa idara ya afya (NHS) ili kupunguza maambukizi katika hospitali, waziri wa Uingereza mwenye dhamana ya chanjo Nadhim Zahawi amesema Jumapili hii.

inafikiria kuifanya chanjo dhidi ya virusi vya Corona  kuwa ya lazima kwa wafanyakazi wa idara ya afya
inafikiria kuifanya chanjo dhidi ya virusi vya Corona kuwa ya lazima kwa wafanyakazi wa idara ya afya AP - Kirsty Wigglesworth
Matangazo ya kibiashara

Uingereza, ambayo ni nchi ya Ulaya iliyoathiriwa zaidi na janga hili, pia ni inaendelea zaidi katika suala la chanjo barani humo na kwa wiki kadhaa imerekodi kesi za kila siku za maambukizi chini ya 5,000.

Lakini hali inazidi kuongezeka na mamlaka ya afya ina wasiwasi juu ya kuesambaa kwa aina mpya ya kirusi kutoka India kilichogunduliwa hivi karibuni, ambacho kimesababisha Boris Johnson kuhoji hatua ya mwisho ya raia kuzuiliwa katika njumba zao, iliyopangwa kutekelezwa Juni 21 nchini Uingereza, ikiwa kinga ya chanjo haitaimarishwa kufikia tarehe hiyo.

"Ni kwa serikali kuwajibika, kuwa na mjadala, kuuliza swali la njia bora ya kuwalinda watu walio katika mazingira magumu zaidi kwa kuhakikisha kuwa wale wanaowajali wanapatiwa chanjo," Nadhim Zahawi amekiambia kituo cha Sky News.

Nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Ufaransa na Ujerumani, zimetangaza kuimarishwa kwa hatua za tahadhari kwa watu wanaowasili kutoka Uingereza, na kwa Ufaransa hatua ya karantini imefanywa kuwa ya lazima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.