Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Johnson ataka tahadhari licha ya kulegezwa kwa masharti dhidi ya COVID-19

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametoa wito kwa raia wa Uingereza kuwa waangalifu wakati hatua kadhaa dhidi ya COVID-19 zikiondolewa nchini humo leo Jumatatu.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, wakati akizuru maabara moja huko Glasgow, Escocia, Januari 28, 2021.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, wakati akizuru maabara moja huko Glasgow, Escocia, Januari 28, 2021. Jeff J Mitchell POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Bw Johnson amebaini kwamba ongezeko la visa vya maambukizi limeripotiwa katika maeneo mengine ya Ulaya na bado kuna tishio linalosababishwa na aina mpya ya kirusi cha Corona.

Kuanzia leo Jumatatu, mikusanyiko ya watu sita au kaya  mbili tofauti inaruhusiwa, wakati viwanja vya michezo vinaweza kutumiwa kwa kuzingatia tahadhari kuhusu matangamano ya kimwili.

Kampeni ya chanjo nchini Uingereza ni moja wapo ya ufanisi zaidi ulimwenguni, lakini wasiwasi unaendelea juu ya usambazaji wa chanjo, viwango vya maambukizi katika sehemu za Ulaya na kuzuka kwa aina mpya ya kirusi cha Corona kinachoambukia haraka.

"Tunapaswa kuwa waangalifu," Boris Johnson amesema. "Licha ya kulegezwa kwa baadhi ya hatua, kila mtu lazima aendelee kuzingatia sheria," ameongeza, akisisitiza umuhimu wa uvaaji wa barakoa na kuheshimu utengamano wa kijamii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.