Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-UTAFITI

Afrika Kusini: Hakuna dalili kwamba kirusi cha Omicron husababisha ugonjwa mbaya zaidi

Wanasayansi wa Afrika Kusini hawaoni dalili kwamba kirusi kipya cha Omicron kinasababisha ugonjwa mbaya zaidi, wametangaza Ijumaa hii Desemba 10.

Ingawa wanasayansi wanasema inachukua muda mrefu kufikia hitimisho la uhakika, Waziri wa Afya Joe Phaahla amesema dalili za agonjwa mahututi wamekutwa wameambukizwa virusi vya Corona.
Ingawa wanasayansi wanasema inachukua muda mrefu kufikia hitimisho la uhakika, Waziri wa Afya Joe Phaahla amesema dalili za agonjwa mahututi wamekutwa wameambukizwa virusi vya Corona. AFP - MICHELE SPATARI
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo, mamlaka inapanga kusambaza nyongeza za chanjo, kwani maambukizo ya kila siku yanakaribia rekodi ya juu.

Ingawa ni kweli kwamba data za hospitali zinaonyesha wagonjwa wanaohusishwa na ugonjwa wa COVID-19 wanaongezeka katika zaidi ya nusu ya majimbo tisa ya nchi hi, ukweli unabaki kuwa vifo haviongezeki kwa kiasi kikubwa. Kwa kuongezea, viashiria kama vile muda wa wastani wa kukaa hospitalini vinatia moyo.

Ingawa wanasayansi wanasema inachukua muda mrefu kufikia hitimisho la uhakika, Waziri wa Afya Joe Phaahla amesema dalili za agonjwa mahututi wamekutwa wameambukizwa virusi vya Corona.

"Takwimu za awali zinaonyesha kwamba wakati idadi ya watu wanaolazwa hospitalini inaongezeka, inaonekana ni kutokana na idadi ya kesi badala ya ukali wa wa aina mpya ya kirusi cha Omicron hii," amesema.

Afrika Kusini iliripoti zaidi ya kesi 22,000 mpya za COVID-19 siku ya Alhamisi, na kuweka rekodi wakati wa mlipuko wa nne wa maambukizi yanayosababishwa na kirusi cha Omicron ukiendelea.

Idadi hii, hata hivyo, ni ya chini kuliko kilele cha zaidi ya kesi 26,000 za kila siku zilizorekodiwa wakati wa mlipuko wa tatu uliosababishwa na aina ya kirusi cha Delta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.