Pata taarifa kuu

Mpango wa kuwazuia watu ambao hawajapata chanjo ya Covid-19 wafutliwa mbali Kenya

Nchini Kenya, Mahakama imesitisha mpango uliokuwa umetangazwa na serikali nchini humo kuwazuia watu ambao watakuwa hawajapata chanjo ya kupambana na virusi vya Covid-19 kutopata huduma za serikali na kuingia katika maeneo ya umma kuanzia tarehe 21 mwezi huu.

Muuguzi na mgonjwa wa Corona, wakiwa nyumbani nchini Kenya Julai 27 2021
Muuguzi na mgonjwa wa Corona, wakiwa nyumbani nchini Kenya Julai 27 2021 Β© Carol Korir
Matangazo ya kibiashara

Jaji wa Mahakama Kuu jijini NairobiΒ Antony Mrima amesitisha utekelezwaji wa mpango huo wa serikali ya Kenya hadi pale kesi iliyowasilishwa na mfanyabishara mmoja anayelalamika kuwa hatua hiyo ni ukiukwaji wa haki za binadamu kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo, itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Mwezi Novemba, serikali kupitia Wizara afya iltangaza kuwa, itakuwa lazima kwa mtu yeyote nchini humo kuonesha cheti kuthibitisha kuwa amepata chanjo, kabla ya kuruhusiwa kupata huduma hospitalini, Shuleni na katika Ofisi za Uhamiaji na utozaji ushuru.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za Binadamu la Human Rights Watch nalo, lililaani mpango huo wa serikali ya Kenya na kutaka utupiliwe mbali kwa kile lilichosema Kenya haikuwa na chanjo za kutosha kuwachanja watu nchini humo kabla ya muda wa mwisho wa Desemba 21.

Mpaka sasa, Kenya, imewachanja watu wazima Milioni 3.2 ambao wamepata dozi kamili sawa na asilimia 12 ya raia wa nchi hiyo, huku watu wengine zaidi ya Laki 2 na Elfu 50 wakiambukizwa na zaidi Elfu tano Mia tatu wakipoteza maisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.