Kenya yapokea dozi 880,000 ya Moderna kutoka Marekani
Kenya imepokea dozi 880,000 ya chanjo ya kuzuia Corona aina ya Moderna, kutoka serikali ya Marekani, chini ya mpango wa Covax ,hii ikiwa mara ya kwanza kwa Moderna kutumika nchini humo.
Imechapishwa:
Waziri wa afya nchini Kenya Mutahi Kagwe ,amesema chanjo hiyo ya Moderna, ni sehemu ya dozi milioni 1.7 ambazo zimetolewa na serikali ya Marekani, kupiga jeki kampeni ya uchomaji chanjo nchini Kenya, ambapo serikali inatazamia kuwachanja watu milioni 10 kufikia mwezi Desemba mwaka huu na wengine miloni 26 kufikia mwezi Juni mwaka ujao.
Aidha amesema dozi zingine karibu laki nne, chanjo aina ya Johnson and Johnson, zinatazamiwa kuwasili nchini juma hili.
Hadi Kenya imechanja asilimia mbili ya raia wake kutumia chanjo ya AstraZenica na hii itakuwa ni mara ya kwanza Kenya itatumia aina nyingine ya chanjo.
Kenya imeripoti maambukizi mapya 646 ndani ya siku moja iliyopita na vifo 30 katika kipindi hichi , hii ikifikisha idade yote ya watu walioambukizwa kufkia lakini mbili ,elfu ishirini mbili na tisa ,watu elfu nne mia nne na tisini na saba wakiwa wamepoteza maisha kutokana na Corona.