Pata taarifa kuu
KENYA

Covid-19: Wafanyakazi ambao hawajachanjwa kuchukuliwa vikwazo Kenya

Kenya imetishia kuwachukulia vikwazo maafisa wake ambao watakuwa hawajachanjwa kabla ya mwishoni mwa mwezi wa Agosti, kulingana na waraka rasmi ambao shirika la habari la AFP limepata kopi.

3% kwa jumla ya wakaazi milioni 47 wa Kenya ndio ambao wamepewa chanjo.
3% kwa jumla ya wakaazi milioni 47 wa Kenya ndio ambao wamepewa chanjo. Simon MAINA AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Wakati Kenya inakabiliwa na mlipuko wa virusi vya Corona, bunge la Kenya linatarajiwa kujadili Alhamisi wiki hii kuhusu marufuku kwa wale ambao hawajachanjwa kufika katika maeneo yao ya kazi. Mjadala huu unafanyika katika mazingira magumu ya kampeni ya chanjo, baada ya 3% kwa jumla ya wakaazi milioni 47 wa nchi hiyo ambao wamepewa chanjo.

"Baadhi ya maafisa wamekwepa kwa makusudi kupewa chanjo," Joseph Kinyua, mkurugenzi wa huduma za umma ameandikia wizara mbalimbali, akisema kuwa upatikanaji wa chanjo "umepelekea hali kuboreka zaidi".

Joseph Kinyua ameongeza kuwa idadi ya watu waliopewa chanjo katika idara za usalama na elimu ni ndogo sana, wakati sekta hizo zinachukuliwa kama taaluma muhimu.

Wale ambao hawajapata dozi yao ya kwanza ya chanjo kufikia Agosti 23 "watachukuliwa hatua za kinidhamu, na hatua zinazofaa zitachukuliwa dhidi yao," ameandika mkurugenzi wa huduma za umma, bila kutoa maelezo zaidi.

Kenya inakusudia kufikia chanjo milioni 26 kufikia mwisho wa mwaka 2022. Zuio la kutotoka nje limeanza tangu mwaka jana, wakati nchi hiyo imerekodi jumla ya maambukizi 213,000 ya Covid-19, na vifo 4,211.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.