Pata taarifa kuu
KENYA-AFYA

Kenya yakabiliwa na uhaba wa chanzo ya AstraZeneca kutoka India

Watu waliopokea chanjo ya kwanza aina ya AstraZeneca kuwazuia dhidi ya maambukizi ya Corona nchini Kenya, watalazimika kusubiri zaidi kupata dozi ya pili, kufuatia uhaba wa chanjo nchini humo.

Daniel Ole Kissipan, anapokea chanjo ya AstraZeneca / Oxford dhidi ya ugonjwa wa Corona (COVID-19) chini ya mpango wa COVAX, jijini Nairobi, Kenya, Aprili 27, 2021.
Daniel Ole Kissipan, anapokea chanjo ya AstraZeneca / Oxford dhidi ya ugonjwa wa Corona (COVID-19) chini ya mpango wa COVAX, jijini Nairobi, Kenya, Aprili 27, 2021. REUTERS - MONICAH MWANGI
Matangazo ya kibiashara

Watu waliokuwa wamepokea dozi ya kwanza, walitarajiwa kupokea dozi ya pili mwezi Juni lakini, uhaba sasa unashuhudiwa baada ya mzalishaji mkubwa wa chanjo aina ya AstraZeneca, nchi ya India, kusitisha usafirishaji wa chanjo hiyo kufuatia ongezeko la maambukizi katika nchi hiyo.

Wizara ya afya nchini Kenya sasa inasema, inaweka mikakati ya kupata chanjo nyingine kwa ajili ya watu wake, hali ambayo sasa inazua wasiwasi nchini humo.

Enock Ocholla, ni miongoni mwa watu waliopewa dozi ya kwanza nchini humo.

 “Huenda tukapatwa na matatizo ya kimwili iwapo tutakosa kupata chanjo ya pili jinsi tulivyokuwa tumehaidiwa, kwa mfano mimi nilipata chanjo ya kwanza tarehe moja mwezi Aprili na nilikuwa natarajia chanjo ya pili tarehe 27 juma lijalo,” amesemaEnock Ocholla, mmoja mwa watu waliopewa dozi ya kwanza nchini Kenya.

Kenya ilipokea chanjo zaidi ya Milioni Moja mwezi Machi, na licha ya kuanza kutolewa, baadhi ya Wakenya bado hawana imani na chanjo, licha ya elimu inayotolewa.

”Sina Imani na chanjo zilizoidhinishwa nchini Kenya, najipa muda kidogo niweze kuona yale madhara yatakayotokana na chanjo hii, ndio niweze kuendea,” amebaini Angose Philip.

Naye Victor Onyino, mtalaam wa afya nchini Kenya, amesema ni muhimu kupata dozi ya pili ya chanjo.

Chanjo ile tulipata kwa mara ya kwanza inaweza kutuzuia kupata janga la corona kwa asilimlia 80 lakini unapoaambiwa upate chanjo ya pili, hiyo tunasema ni muhimu zaidi, ina maanisha kwamba inaongezea uwezo wake wa kuzuia kupata janga la corona kwa hadi asilimia 90.

Tumaini la Wakenya sasa ni kwa serikali yao, ambayo imewaambia waendelee kusubiri chanjo zaidi kuingia nchini humo, lakini mpaka sasa haifahamiki ni lini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.