Pata taarifa kuu
KENYA-COVID 19

Kampeni ya utoaji chanjo nchini Kenya huku maambukizi yakiongezeka

Kenya imeongeza masharti ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona kwa siku 60 zaidi, ikiwa ni pamoja na kuzuia mikusanyiko ya kisiasa lakini pia muda wa watu kutembea nje kati ya saa nne usiku mpaka saa 10 Alfajiri.

Afisa wa afya akitoa chanjo kwa raia wa Kenya
Afisa wa afya akitoa chanjo kwa raia wa Kenya REUTERS - MONICAH MWANGI
Matangazo ya kibiashara

Katika hatua nyingine, kmapeni ya kutoa chanjo kwa watu nchini humo inaendelea ili kupambana na ongezeko la maambukizi hayo.

Mwandishi wetu Hillary Ingati ameshuhudia namna watu wanavyopokea chanjo katika mitaa ya jiji la Nairobi, hii hapa ripoti yake.

Mtaa wa Dandora Mashariki mwa jiji la Nairobi, kuna foleni ndefu ya watu walioitia wito wa serikali ya Kenya, kuja kupokea chanjo aina ya AstraZeneca inayotolewa bure.

Sarah Depa mkaazi wa mtaa huu wa Dandora phase 1, baada ya kupanga foleni amefanikiwa kuchoma chanjo.

“Ndio nimepokea jab yangu ya kwanza na niko sawa hakuna kitu nichokisikia, sababu yangu ya kuchanjwa ni ilikuzuia wale ambao niko karibu na wao na kwa sababu ya afya yangu, ”

Mita chache na eneo la kutolea chanjo, nakutana na vijana wawili wa kiume, wanaeleza ni kwanini wanasita kwenda kupata chanjo.

“Leo niliaamkia mahali wanapatiana chanjo na nikapata foleni ni kubwa watu ni wengi pia masaa yenye wanaanza kutoa hiyo chanjo ni mbaya sana wanachelewa sana unawezapoteza kibarua,”

“Sababu kubwa ya kutopata chanjo ni masaa, mimi hufanyia kazi kwa nyumba na kufunga kwenda huko kupata chanjo inachukua muda mrefu.”

Mary Muchomba NI mhudumu wa afya kwenye kituo hiki anaelezea changamoto na mwitikio wa watu.

“Tunapata idadi kubwa ya watu amabo wanakujia chanjo wakati huu na ni wingi kuliko idadi yetu wahudumu wa afya ambao tuko hapa pia watu hawataki kucoperate na sisi.” amesema.

Wizara ya afya nchini Kenya, inasema mpaka sasa ni watu zaidi ya Milioni Mbili ndio waliopokea chanjo, katika taifa hilo la watu zaidi ya Milioni 52.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.